logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Mpenzi wangu wa kweli wa kwanza, Nakumiss!' Wema Sepetu amsherehekea marehemu baba yake

Bw Sepetu aliaga mwaka wa  2013 baada ya kupambana na ugonjwa wa kisukari na kiharusi

image
na Radio Jambo

Habari16 October 2022 - 11:31

Muhtasari


•Muigizaji Wema Sepetu ametumia siku ya leo kumkumbuka marehemu baba yake na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

•"Endelea kupumzika baba angu mimi.. Nakupenda kila siku .. Nakumiss kila siku.. Nakumiss kila wakati.. Naendelea kukuombea sana," alisema.

katika picha ya maktaba.

Siku kama ya leo, baba ya muigizaji wa Bongo Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu angekuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Bw Sepetu ambaye aliaga dunia takriban miaka tisa iliyopita alizaliwa Oktoba 16, miongo mingi iliyopita. Alifariki mnamo tarehe 27 Oktoba mwaka wa  2013 baada ya kupambana na ugonjwa wa kisukari na kiharusi kwa kipindi kirefu.

Muigizaji Wema Sepetu ametumia siku ya leo kumkumbuka marehemu baba yake na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa mwenzangu wa Libra, baba yangu Sepetu.. Mpenzi wangu halisi wa kwanza," aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mpenzi huyo wa mwimbaji Whozu alimtakia marehemu babake mapumziko ya amani na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Endelea kupumzika baba angu mimi.. Nakupenda kila siku .. Nakumiss kila siku.. Nakumiss kila wakati.. Naendelea kukuombea sana," alisema.

Aliongeza "Allah akupunguzie adhabu za kaburi.. Amen🙏🙏🙏❤❤❤,"

Muigizaji huyo aliambatanisha ujumbe wake na picha kadhaa za kumbukumbu za mzazi huyo wake ambaye aliaga.

Bw Sepetu alifariki katika  hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, Tanzania ambako alikuwa akipokea matibabu. Baada ya kuaga, marehemu alizikwa nyumbani kwake katika  maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar es Salam.

Bw Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika miaka ya 1970 wakati wa utawala wa muhula wa kwanza wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.

Kufikia kufariki kwake, Bw Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved