logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Boris Johnson ajiondoa kwenye mbio za uwaziri mkuu Uingereza

Johnson amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwa kiongozi wa chama cha Conservative na waziri mkuu ajaye wa Uingereza.

image
na Radio Jambo

Michezo24 October 2022 - 03:54

Boris Johnson amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwa kiongozi wa chama cha Conservative na waziri mkuu ajaye wa Uingereza.

Hii hapa taarifa yake kamili kujiondoa:

Katika siku chache zilizopita nimeelemewa na idadi kubwa ya watu waliotakaa nigombee tena uongozi wa Chama cha Conservative, miongoni mwao ni marafiki na wafanyakazi wenzangu Bungeni. Nimevutiwa kwa sababu niliongoza chama chetu katika ushindi mkubwa wa uchaguzi miaka mitatu iliyopita - na ninaamini kwamba hivyo nina nafasi ya kipekee wa kuepusha uchaguzi mkuu kufanyika sasa.

Uchaguzi mkuu utakuwa usumbufu zaidi pale ambapo Serikali lazima izingatie shinikizo za kiuchumi zinazokabili familia kote nchini.

Ninaamini niko katika nafasi nzuri ya kuipa ushindi Conservative katika uchaguzi wa 2024 - na usiku wa leo ninaweza kuthibitisha kambwa nitapeleka jina langu kwa uteuzi kesho.

Kuna nafasi nzuri sana kwamba ningeshinda katika uchaguzi wa Chama cha Conservative - na kwamba kwa kweli ningeweza kurudi Downing Street siku ya Ijumaa.

Lakini katika kipindi cha siku za mwisho nimefikia hitimisho la kusikitisha kwamba hili halingekuwa jambo sahihi kufanya kwa saaa.

Huwezi kutawala ipasavyo isipokuwa uwe na chama chenye umoja bungeni.

Na ingawa nimewasiliana na Rishi (Sunak) na Penny (Mordaunt) - kwa sababu nilitumaini kwamba tunaweza kuja pamoja kwa maslahi ya taifa - kwa masikitiko makubwa hatujaweza kutafuta njia ya kufanya katika hili.

Kwa hivyo ninaogopa, jambo bora zaidi ni kwamba uteuzi wangu kupelekwa hatua za mbele (najiondo) na nitamuunga mkono yeyote atakayefanikiwa.

Ninaamini nina mengi ya kusaidia lakini ninaogopa kuwa huu sio wakati sahihi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved