logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nataka mtoto mwingine ndio nifunge ukurasa kabisa - Karen Nyamu

Kuwa na mtoto katika ua la nyumba yako ni moja kati ya Baraka kubwa sana maishani. - Nyamu.

image
na Radio Jambo

Habari24 October 2022 - 11:21

Muhtasari


• Nyamu na Samidoh tayari wana watoto wawili pamoja.

Nyamu asema anataka mtoto mwingine

Seneta maalum Karen Nyamu amedokeza kutafuta mtoto wa tatu ambaye atakuwa wa mwisho kabla ya kufunga kabisa ukurasa wa kuwa mjamzito tena.

Kupitia insastories zake, Nyamu alipakia picha ya mwanamke mmoja akiwa ameshika mtoto na kuachia maoni kwamba kuwa na mtoto katika ua la nyumba yako ni jambo moja ambalo kina mama analionea fahari sana.

Katika picha hiyo inayodhaniwa kuwa yaya wake ambaye alikuwa amemshika mwanawe, Nyamu alisema kwamba furaha ya kuwa mama ndio itakayomfanya kutafuta mtoto mwingine wa mwisho kabisa na kufunga uzazi.

“Kuwa na mtoto katika ua la nyumba yako ni moja kati ya Baraka kubwa sana maishani. Ninataka mmoja wa mwisho ndio nifunge ukurasa kabisa,” Karen Nyamu alidokeza.

Mama huyo ana watoto watatu tayari, wawili akiwa amewazaa na mwanamuziki Samidoh na ni kama lengo lake ni kufikisha watoto wane, kulingana na ujumbe huo aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Samidoh na Nyamu walimkaribisha mtoto wao wa pili mapema mwaka huu na kuonekana kutokuwa pamoja baada ya kurushiana cheche kwa njia fiche kupitia mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni, inadaiwa wawili hao tena wamerudiana, baada ya Samidoh kuonekana kwenye bunge la seneti wakati Nyamu alikuwa anaapishwa kama seneta mteule.

Samidoh alionekana kweney majengo ya bunge akiwa na wanawe wawili ambao amezaa na Nyamu na wiki jana alipokuwa anaondoka kwenda ziara ya kimuziki Marekani, Nyamu alipakia ujumbe kwenye Instagram yake akidokeza kwamba yeye na watoto wake watakmosa sana msanii huyo ambaye anatarajiwa kutumbuiza Marekani kwa wiki kadhaa zijazo.

Hata hivyo, hakusema anataka kuzaa na nani mtoto huyo wa nne.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved