logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alinyoa, akauza wigi ili kuninunulia saa - Mitindo aeleza sababu ya kumpenda Wolper

Nilivyofika nyumbani nikakuta amekata nywele zote na ameuza wigi kuninunulia saa mpya - Mitindo alisema.

image
na Radio Jambo

Habari27 October 2022 - 08:41

Muhtasari


• "Cha kujifunza katika hii hadithi, kupenda si kitu, kupendwa ni kitu ila kupenda na ukapendwa na umpendaye hiyo ndio kila kitu," - Mitindo alishauri.

Mitindo afunguka kwa nini anampenda Wolper

Rich Mitindo, mfanyibiashara wa nguo ambaye pia ni mbunifu wa nguo za wanaume ametoa sababu za kwa nini anampenda mwigizaji Jacqueline Wolper.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mitindo ambaye kwa muda wa siku kadhaa sasa amekuwa akidokeza kuwepo kwa harusi yake na Wolper hivi karibuni aliweka kila kitu bayana ili wambea wajue sababu za penzi lake kuota katika moyo wa mwigizaji Wolper.

Alisema kwamba sababu kuwa Wolper tayari amemzalia watoto wawili tayari sio ya kipekee kumfanya kumpenda bali alisimulia pia tukio moja ambalo lilimfanya kuzidisha upendo wake kwa Wolper pasi na kikomo.

Mitindo alisimulia siku moja mpenzi wake huyo alipomtaka kumnunulia wigi ila akawa hana pesa na hata kutaka kuiuza saa yake ya mkononi ambayo ilikuwa imevunjika ili kukidhi hitaji la wigi kwa Wolper.

Swali kwanini namuoa nakumpenda Mama P? Ukiacha kunizalia sababu nyingine hii hapa. Kuna Siku Mama P alikuwa anahitaji hela ya nimnulilie wigi jipya nikamwambia Sina hela unaona hata Saa yangu nayoipenda imevunjika nashindwa hata kununua mpya😌 Ila nilivyotoka kwenda kazini kuna jamaa alitaka saa yangu hiyo hiyo ambayo imepasuka ikabidi niuze hela nimchukulie mpenzi wangu wigi jipya,” Mitindo alifunguka tukio hilo ambalo halijawahi kusimuliwa na yeyote.

Alipofika nyumbani alipigwa na mshangao kumuona Mama P kama anavyojiita Wolper amezikata nywele zote na wigi la zamani kuliuza kwa rafiki yake, pesa akaenda kumchukulia saa mpya mpenzi wake!

“Nilivyofika nyumbani nikakuta amekata nywele zote na ameuza wigi ambalo analipenda kwa shoga yake hela akaenda kunichukulia Mimi saaa Mpya. Cha kujifunza katika hii story KUPENDA SI KITU, KUPENDWA NI KITU ILA KUPENDA NA UKAPENDWA NA UMPENDAYE HIYO NDO KILA KITU🙏 Kamwe usichukulie upendo kiurahisi👏” Mitindo alimaliza kwa ushauri kuntu kweli.

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved