logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtu ambaye hajawahi nisaliti ni mama, shenzi sana kama humthamini mamako - Prezzo

Mazuzu wame Pata dili la laki moja, wanatuma elfu kumi kwa mama zao ila kwa Dem wanatuma elfu tisini iliyobaki - Prezzo.

image
na Radio Jambo

Habari02 November 2022 - 10:26

Muhtasari


• “Mama ndio dhahabu,” mtangazaji Clemmo254 alikubaliana naye.

Prezzo na mamake

Mwanamuziki mkongwe katika Sanaa ya nchini Kenya Prezzo amewasuta wanaume ambao wanatumia pesa ndefu katika kuwafurahisha wapenzi wao na wakati huo huo kutumia kiasi finyu kuwaridhisha kina mama zao.

Kupitia video fupi aliyoipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mamake ndani ya gari, msanii huyo aliweka wazi kwamba mtu pekee katika maisha haya ambaye hajamsaliti ni mama yake mzazi.

Mtu ambae hajanisaliti tu ni Mama. Mazuzu wame Pata dili la laki moja, wanatuma elfu kumi kwa mama zao ila kwa Dem wanatuma elfu tisini iliyobaki 🙆🏽️ shenzi kabika!” Prezzo alisema.

Katika klipu hiyo, Prezzo na mamake walionekana kuwa na wakati mzuri ndani ya gari lake huku msanii huyo ameketi nyuma ya bomba na mamake kiti cha nyuma wakiwa na mazungumzo ya mama kwa mwanawe.

Mashabiki wake wengi walionekana kukubaliana na kauli yake huku wakisema kuwa hakuna thawabu iliyo na utukufu wa kudumu kama thawabu kutoka kwa tamko la mama akikuambia ahsante baada ya kumfanyia kitu.

“Mama ndio dhahabu,” mtangazaji Clemmo254 alikubaliana naye.

 Hata hivo, wapo wengine waliokuwa na mtizamo hasi kuhusu kauli yake kuwataka watu kuwaweka mama mbele kabla ya mpenzi.

Wengine walimwambia kwamba si vizuri kuendekeza wazazi kila muda kwani wakati mwingine mtu ukishakomaa basi unafaa kujijenga mwenyewe na familia ya kwako huru pia.

“Kwani utakuwa unafanyia mamako? Unafaa kujijenga pia,” mmoja kwa jina Nelson alisema.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved