logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini Bahati hakuwa kwenye thieta wakati wa kuzaliwa kwa bintiye Heaven

Alimdanganya Diana kuwa wanaume hawakuruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kujifungulia.

image
na Radio Jambo

Habari07 November 2022 - 04:50

Muhtasari


•Baba huyo wa watoto watano alisema hangeweza kustahimili kuwa katika chumba cha kujifungua wakati huo.

•Bahati alisema tangu wakati huo amepamba na hilo na alikuwepo wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wao wa tatu hivi majuzi.

Bahati alimdanganya mke wake Diana Marua kwamba madaktari walimkataza kuwa katika chumba cha kujifungulia alipokuwa akimkaribisha mtoto wake wa kwanza na Marua, Heaven Bahati.

Akizungumza kwenye YouTube Channel ya Diana, baba huyo wa watoto watano alisema hangeweza kustahimili kuwa katika chumba cha kujifungua wakati huo.

"Walinitaka niingie ndani lakini nilikataa na nikamwambia amwambie Diana kuwa hawakuruhusu wanaume kuingia thieta," alisema.

Bahati alisema alisubiri nje huku akiwaza la kufanya.

"Niliogopa hata kumshika mtoto wangu mnamo siku ya kwanza," alisema.

Bahati alisema tangu wakati huo amepamba na hilo na alikuwepo wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wao wa tatu hivi majuzi.

Diana alimkaribisha mtoto wake, Malkia Bahati, siku tano kabla ya siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake. Alitimiza miaka 33.

Wakati wa siku yake ya kuzaliwa, Bahati alisema yeye ndiye mwanamke aliyeyapa maisha yake maana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved