logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume anayeshukiwa kumuua mpenziwe Lang'ata akamatwa katika mpaka wa Malaba

Thomas Mbugua Muthee alinaswa na wapelelezi katika mpaka wa Malaba

image
na Radio Jambo

Habari18 November 2022 - 22:29

Muhtasari


  • Atashtakiwa kwa mauaji kinyume na kifungu cha 203 kama inavyosomwa na kifungu cha 204 cha kanuni ya adhabu

Mwanamume anayeshukiwa kumuua mpenzi wake katika mtaa wa Onyonka, Nairobi, wiki jana amekamatwa.

Thomas Mbugua Muthee alinaswa na wapelelezi katika mpaka wa Malaba alipokuwa akijaribu kutoroka nje ya nchi hadi nchi jirani ya Uganda.

Mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa mafichoni tangu atekeleze kitendo hicho cha kinyama Jumamosi wiki iliyopita kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi Malaba. Atahamishiwa Nairobi siku ya Jumamosi.

Atashtakiwa kwa mauaji kinyume na kifungu cha 203 kama inavyosomwa na kifungu cha 204 cha kanuni ya adhabu.

“Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kikatili ya Naneu Muthoni, aliyepatikana ameuawa katika nyumba yake mnamo Novemba 14, mtaa wa Onyoka katika kaunti ndogo ya Langata amekamatwa.

Kituo cha Polisi cha Malaba kabla ya kuhamishiwa kituo cha polisi cha Langata, ambako atafunguliwa mashtaka ya mauaji kinyume na kifungu cha 203 kama inavyosomwa na kifungu cha 204 cha kanuni ya adhabu na kufikishwa mahakamani kujibu makosa yake," ilisema taarifa kutoka DCI.

Ripoti ya uchunguzi wa maiti ya Naneu Muthoni, aliyepatikana ameuawa katika eneo la Lang'ata mnamo Jumatatu ilifichua kwamba alifariki kutokana na jeraha la ubongo.

Ripoti hiyo pia ilifichua kwamba alipigwa mara kadhaa kwa kitu butu na kitu chenye ncha kali kikapenya kichwani mwake.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved