logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Awinja afungua biashara ya mukombero, sim sim na njugu karanga Qatar (+Video)

Muigizaji huyo likuwa akiwauzia mashabiki  kwa shilingi 20 pekee.

image
na Radio Jambo

Habari28 November 2022 - 12:12

Muhtasari


• Awinja ambaye alifadhiliwa kuenda Qatar na kampuni moja ya kamari ya hapa nchini pia anaonekana akijaribu kuuza simsim na njugu karanga kwa mashabiki.

• Awinja, ambaye jina halisi ni Jacky Vike, alipatwa kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kitendo hicho.

Muigizaji maarufu Awinja Nyamwalo amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana  katika uwanja mmoja wa Qatar akiuza mukhombero kwa mashabiki waliohudhuria mechi kati ya Morocco na Ubelgiji.

Katika video ambayo imesambwa sana kwenye mitandao ya kijamii, Awinja ambaye alifadhiliwa kuenda Qatar na kampuni moja ya kamari ya hapa nchini pia anaonekana akijaribu kuuza simsim na njugu karanga kwa mashabiki.

Huku mashabiki wa timu ya Morocco wakiwa wamejazana uwanja hadi pomoni, Awinja alikuwa anawauzia bidhaa hizo ambazo ni maarufu Kenya alizokuwa kwa shilingi 20 pekee.

Mashabiki waliokuja kujionea mechi hiyo kali walionekana kwenye video wakionja na kufurahia bidhaa hizo ambazo ni maarufu nchini Kenya.

“Nimekuja hapa kuwasaidia. Huu ni mmea ambao unasaidia kuongeza msisimko wakati wa mapenzi kutoka Kenya'' Awinja alisikika akisema huku mashabiki wakimjongea na kuzionja bidhaa hizo.

Baada ya kuonja, baadhi ya mashabiki walionekana kupendezwa huku wengine wakisikika wakisema kuwa “Naipenda!”.

Awinja, ambaye jina halisi ni Jacky Vike, alipatwa kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kitendo hicho.

Mwanamitandao mmoja alisema ''Huyo sasa alifikishaje mkombelo Qatar''

Mwanamitandao wa pili alisema '' Mpaka njungu, awinja weka sema mahali uko tuje''


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved