logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke Mkenya, binti zake wawili wauawa na mumewe Marekani

Watatu hao waliuawa kwa kupigwa risasi kabla ya mumewe kujitoa uhai.

image
na

Habari05 December 2022 - 07:11

Muhtasari


• Bw Gary Stanton alijitoa uhai baada ya kutekeleza mauaji hayo nyumbani kwao katika mtaa wa Valley Station, jijini  Louisville.

•Polisi wametaja kisa hicho kuwa mauaji ya kinyumbani.

Familia iliyouawa Marekeni

Polisi nchini Marekani wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja Mkenya aliuawa pamoja na watoto wake wawili na baadaye mume wake akajitoa uhai katika mtaa wa Valley Station, jijini  Louisville.

Mwanamke huyo aliyetambulishwa kama Njoki Muchemi Stanton, mwenye umri wa miaka 49,  alipatikana amekufa kando ya mumewe, Gary Stanton mwenye umri wa miaka 60. Wote walikuwa na majeraha ya risasi.

Mabinti wake, Muchemi Andrianna Stanton mwenye umri wa miaka 17 na Brianna Stanton mwenye umri wa miaka 11, pia walipatikana wakiwa wameaga dunia.

Polisi wametaja kisa hicho kuwa mauaji ya kinyumbani, wakisema waathiriwa wote walikuwa wa familia moja.

Huku uchunguzi zaidi wa Kitengo cha Mauaji cha LMPD ukiendelea, inaripotiwa kuwa mwanamume huyo ndiye aliyetekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Maelezo kwenye ukurasa wa Facebook wa marehemu Njoki yanadokeza kwamba  alikuwa amesherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi majuzi ambapo mumewe  Gary alimtakia heri  ya siku ya kuzaliwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved