Mapacha 9 kutoka Mali wameingia kwenye rekodi ya dunia baada yao kuorodheshwa kama watoto waliowahi kuzaliwa mara moja na kuishi wote.
Kulingana na BBC, mapacha hao waliingia kwenye rekodi hiyo ya Guinness Book of Record baada ya kuzaliwa mnamo Mei mwaka wa 2021 nchini Morocco.
Waliwekwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa miezi 19 baada ya kurejeshwa nyumbani wakiwa na mama yao.
Mama ya watoto hao Halima Cisse mwenye umri wa miaka 27, kabla ya kurejea alikuwa amepelekwa katika jiji la Casablanca nchini Morocco kwa ajili ya uangalizi maalum na watoto wake 9.
Baba ya watoto hao Abdelkader Arby aliyekuwa amejawa na furaha, aliwapokea mama na watoto wake kwenye uwaja wa ndege baada ya kutua salama mji mkuu wa Mali, Bamako.
Arby huku akiwa amejawa na tabasamu kuu alishukuru serikali ya Mali ambayo ilikuwa ikitoa ufahdili wa kifedha kwa familia hiyo muda wote. Serikali ya Mali iliahidi zaidi kusaidia familia hiyo kwa malezi ya watoto hao.
'' Ni kazi kubwa lakini Mwenyezi Mungu aliyetupa baraka hii atatusaidia katika malezi yao na kuwatunza.'' Mwanaume huyo alisema.
Alisema watoto hao ni mapacha waliotofautiana kitabia kwani wengine wako kimya wengine wanapiga kelele zaidi na wengine wanalia sana. Wengine wanapenda sana kushikwa kila wakati. Wote ni tofauti sana, ambayo hiyo sana.
Bw Arby pia alisema watu wengi wanatoka mbali kuenda kuwaona watoto wao
Mama Cisse ambaye alijifungua watoto hao kwa njia ya upasuaji, alijaliwa wasichana watano na wavulana wanne kwa wakati mmoja.