logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto atuma risala za rambirambi kwa familia ya wakili Ahmednasir baada ya kumpoteza mama yake

Waziri wa Ulinzi Aden Duale pia alituma ujumbe wa rambirambi kwa familia.

image
na Radio Jambo

Michezo27 December 2022 - 17:02

Muhtasari


  • Rais William Ruto mnamo Jumanne alituma ujumbe wa rambirambi kwa familia ya Wakili Mkuu na kuomba kwamba familia hiyo ipate nguvu wakati wa maombolezo
Star, KWA HISANI

Wakili Mkuu Ahmednasir Abdullahi na familia yake wako katika maombolezo kufuatia kifo cha mamake, Mama Saado Ahmednoor.

Rais William Ruto mnamo Jumanne alituma ujumbe wa rambirambi kwa familia ya Wakili Mkuu na kuomba kwamba familia hiyo ipate nguvu wakati wa maombolezo.

"Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Raji'un. Natoa pole nyingi kwa Ahmednasir Abdullahi, kufuatia kuondokewa na mama yako, Saado Ahmednoor. Nakuombea rehema za Mwenyezi Mungu wewe na familia na rehema za Mwenyezi Mungu na amani kwa roho ya Mama Saado," alisema.

Waziri wa Ulinzi Aden Duale pia alituma ujumbe wa rambirambi kwa familia.

"Kwa niaba ya familia yangu na mimi mwenyewe, ninatuma salamu zangu kwa familia na marafiki wa kaka yangu Ahmednasir kwa kifo cha Mama Saado Ahmed Noor; mama yake na bibi yetu," alisema.

Ewe Mwenyezi Mungu, wasamehe walio hai wetu na wafu wetu, waliopo na wasiokuwepo, vijana wetu na wazee wetu, wanaume wetu na wanawake wetu. Ewe Mwenyezi Mungu ambaye unamuweka hai miongoni mwetu, basi maisha kama hayo yawe juu ya Uislamu, na ambaye unamchukua miongoni mwetu kwa nafsi Yako, basi kifo hicho kiwe juu ya imani."

Wakili Ahmednasir alikuwa bado hajatoa taarifa kwa umma kuhusu kifo cha mamake.

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved