logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nelson Havi:Si jambo la busara kwa mbunge kubuni kutengwa kwa mawakili kwenye tume za kikatiba

Kulingana na Nelson Havi si jambo la busara kwa mbunge kutafakari na kubuni kutengwa kwa wanasheria

image
na Radio Jambo

Habari19 January 2023 - 11:11

Muhtasari


  • Kulingana na Nelson Havi si jambo la busara kwa mbunge kutafakari na kubuni kutengwa kwa wanasheria kutoka kwa tume za kikatiba au jopo la uteuzi wa wanachama wao
Wakili Havi atetea ukimya wake siku za hivi karibuni

Aliyekuwa Rais wa chama cha mawakili nchini LSK Nelson Havi ameonya hatua ya hivi punde ya wabunge kuwatenga mawakili katika masuala ya kikatiba.

Kulingana na Nelson Havi si jambo la busara kwa mbunge kutafakari na kubuni kutengwa kwa wanasheria kutoka kwa tume za kikatiba au jopo la uteuzi wa wanachama wao.

Havi alisema kwamba hamna mtu mwingine mbali na mwanasheria ana nafasi nzuri ya kushauri katika tafsiri na utekelezaji wa Katiba.

"Si jambo la busara kwa mbunge kutafakari na kubuni kutengwa kwa mawakili kwenye tume za kikatiba au jopo la uteuzi wa wanachama wao."

Havi  aliendelea na kuuliza;

Nani zaidi ya mwanasheria ana nafasi nzuri ya kushauri katika tafsiri na utekelezaji wa Katiba na sheria?"Alisema Havi.

Wakenya walitoa maoni yao baada ya matamshi ya Havi, na haya hapa baadhi ya maoni yao;

Balasundram Ravindran: When you were entering politics and chose to contest for an MP seat, I and many others warned you politics wasn't for you. Politicians hate to see people with conscience working for them. It's coz of that reason people like you and Miguna were not invited to take up any position.

Ndong: On this I agree with you. There is an URGENT NEED to include the LSK in that Panel by all standards. Now that PSC are all President's appointees. I do not see any legal, policy or practical reason why they should have a slot. PERIOD!

sam waweruh: We are having so many professionals being isolated from business deals and transactions


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved