logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uganda: Mashabiki wa Arsenal wakatamwa wakisherehekea ushindi dhidi ya Man U

Inaarifiwa walitatiza shughuli katika jiji la Jinja kupelekea polisi kuingilia kati.

image
na Radio Jambo

Habari23 January 2023 - 12:39

Muhtasari


• Arsenal iliibuka mshindi kwa mabaoo 3-2, bao la ushindi likifungwa kunako dakika za lala salama na Nketiah.

Mashabiki wa Arsenal

Jumapili usiku dunia mzima ilikongamana mbele ya runinga, wengine kando ya redio na waliobahatika zaidi kuhudhuria uwanjani Emirates kufuatilia moja kwa moja mechi kubwa kabisa ya wikendi iliyozihusisha timu mbili kubwa katika historia ya ligi ya Premia Uingereza – Arsenali na Manchester United.

Mechi hiyo yenye ilikuwa na ushindani na mihemko ya aina yake iliibua kumbukumbu za miaka ya mapema 2000 wakati United ilikuwa inaongozwa na Sir Alex Ferguson na Arsenal wakiongozwa na Arsene Wenger, mtanange baina yao ulikuwa ni wa kusimamisha mji, mtoto hatumwi dukani, jicho halipepeswi!

Arsenal walikuwa na bahati baada ya kuibuka washindi kwa bao la dakika za zima taa tulale na kutanua pengo hadi alama 5 kileleni mwa jedwali.

Nchini Uganda, mashabiki wa timu hiyo ya London walipeleka mbwembwe zao katika kiwango kingine ambapo waliundwa gwaride la kubuni kuonesha taji lao ambalo walikuwa wanaigiza matukio wakati timu inakabidhiwa taji la ushindi.

Jarida la Daily Monitor liliripoti kuwa gwaride hilo lao lilitatiza shughuli za kawaida katika mji wa Jinja jambo ambalo lilifanya polisi kuingilia kati na kuwatia mbaroni mashabiki zaidi ya 20 wa Arsenal.

Wakati Polisi wakiwa hawajazungumzia tukio hilo, Baker Kasule ambaye alikuwa katika kundi hilo, alimweleza mwandishi wa habari wa Daily Monitor kuwa gari la askari wa doria lilisimama mbele yao na kuwataka kila mmoja kushuka na kupanda gari la doria lililokuwa likielekea Jinja. Kituo cha polisi.

"Sijui tumefanya nini lakini tulikuwa tukisherehekea ushindi wetu dhidi ya wapinzani wetu Manchester United," Bw Kasule alisema na kuongeza kuwa "ni wafuasi 20 kwa jumla, wote kutoka Jinja City."

Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Polisi cha Jinja, Maurice Niyonzima, alikataa kuzungumzia suala hilo, akisema Jeshi hilo lina msemaji.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved