logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siamini katika Valentine's! Jaji Ian afunguka kwa nini hajawahi kuadhimisha siku ya Wapendanao

"Valentine's ni nini? Unasherehekea upendo kila siku. Siku 365,” alisema.

image
na Radio Jambo

Michezo15 February 2023 - 04:35

Muhtasari


•Mbugua ambaye anakumbukwa sana kama jaji asiye na upuuzi  alisema kuwa haamini katika Valentine's.

•Alibainisha kuwa Men's Conference inakusudiwa kutengenezea jukwaa la kueleza masuala yanayohusu wanaume.

Aliyekuwa jaji wa Tusker Project Fame, Ian Mbugua, amefichua kuwa hajawahi kusherehekea Siku ya Wapendanao almaarufu Valentine’s.

Akizungumza na mwandishi Samuel Maina, Mbugua ambaye anakumbukwa sana kama jaji asiye na upuuzi katika shindano hilo la uimbaji ambalo limesitishwa kwa sasa alisema kuwa haamini katika Valentine's.

"Valentine's ni nini? Unasherehekea upendo kila siku. Siku 365,” alisema.

Mwalimu huyo wa muziki pia aliweka wazi kuwa hakuwa na mpango wa kusherehekea Siku ya Wapendanao mwaka huu kwa njia yoyote maalum.

Mbugua alikuwa mmoja wa Wanajopo katika Kongamano la Wanaume (Men’s Conference) la mwaka huu lililofanyika Carnivore Simba Saloon siku ya Jumanne. Alipuuzilia mbali dhana kwamba hafla hiyo inalenga kuipuuza Siku ya Wapendanao.

Akizungumza kuhusu tukio hilo la kila mwaka, alibainisha kuwa linakusudiwa kutengenezea jukwaa la kueleza masuala yanayohusu wanaume.

"Mkutano wa Wanaume ni wanaume tu kuja pamoja na kujadili mambo yanayohusiana na wanaume. Hiyo ndiyo yote. Haina uhusiano wowote na Valentine’s. Wanaume wanaokuja pamoja ili kubadilishana mambo yao na kuuliza maswali,” alisema.

Mkufunzi huyo mashuhuri wa muziki pia alitumia Siku ya Wapendanao kuwahimiza wanaume kutafuta usaidizi wakati wowote wanapokumbana na matatizo ya afya ya akili. Aliwataka wanaume kutokwepa kutafuta mtaalamu au mtu wanayemwamini ambaye wanaweza kumueleza matatizo yao.

"Ni juu yao (wanaume) kuamua. Wanapaswa kujiuliza, je, nahitaji msaada au la? Na ikiwa ninahitaji msaada, ninaweza kupata kutoka wapi? Ni watu waliofunzwa kufanya hivi. Wapo washauri; kuna wanasaikolojia ambao wamefunzwa kwa hili. Hiyo ndiyo kazi yao. Tafuta mmoja na utafute msaada,”

Alipoulizwa ikiwa kuna makosa ya kimaisha aliyoyafanya enzi za ujana wake, Mbugua alibainisha kuwa hakuwa na majuto maishani, ila masomo tu.

Mbugua alikuwa miongoni mwa wageni na wazungumzaji wakuu katika Kongamano la Wanaume 2023 lililofanyika Jumanne. Wageni wengine ni pamoja na Mwanahabari Stephen Letoo, Mtangazaji Swaleh Mdoe, wakili Danstan Omari, Mchekeshaji Dkt. Ofweneke, Dkt Frank Njenga, Robert Alai, Shaffie Weru, Pastor S na Chris Kirwa.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved