logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vijana wenye ushawishi Afrika: Diamond, Harmonize nje; Mbosso, Zuchu ndani!

Rayvanny, Harmonize, Diamond licha ya kumiliki lebo, hawakutajwa kama wenye ushawishi.

image
na Radio Jambo

Habari15 February 2023 - 06:34

Muhtasari


• Wengi wamekuwa na dhana tofauti kuhusu ni kwa nini Diamond, Rayvanny na Harmonize wote walitemwa licha ya kumiliki lebo kubwa.

• Hata hivyo, baadhi ya Wakenya pia walihisi bingwa wa mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge angekuwa kweney orodha hiyo, hakuwepo.

Waafrika vijana wenye ushawishi mkubwa 2022.

Kampuni ya habari kutoka Magharibi mwa Afrika kwa jina Avance Media imetoa orodha ya vijana 100 katika bara la Afrika ambao walikuwa na ushawishi mkubwa mwaka 2022.

Katika orodha hiyo, taifa la Nigeria limeongoza kwa kuwa na vijana 31. Kenya imewakilishwa na vijana 11 huku Tanzania wakiwa na vijana 7 kwenye orodha hiyo.

 Katika orodha hiyo, vijana wa kike waliokuwa na ushawishi mkubwa Afrika nan je ya Afrika ni 43 huku wale wa kiume wakiwa 57.

Hata hivyo, suala kubwa si hilo. Mjadala mkubwa umejikita pale kwa vijana haswa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambao hawakuonekana kwenye orodha hiyo licha ya wengi kudhani wana ushawishi mkubwa.

Kwa mfano kutoka Tanzania, vijana kama vile Harmonize, Rayvanny, Alikiba na Diamond hakuna hata mmoja aliyejinafasi kwenye orodha hiyo, licha ya kila mmoja wao kuwa na lebo ya muziki na kudhaniwa kufanya vizuri Zaidi kimuziki hadi kuvutia ushawishi mwingi.

Badala yake, malimbukeni kama mchekeshaji Kili Paul, Zuchu, Mbosso, Jokate, Barbara Gonzalez, Millard Ayo ndio waliwakilisha taifa hilo kwenye orodha hiyo.

Kutoka nchini Kenya, angalau orodha hiyo iliwiana na matarajio ya wengi baada ya kuwaorodhesha Wakenya walioandikisha rekodi za kusisimua mwaka 2022.

Kwenye orodha hiyo, Wakenya kama mchezaji chipukizi wa tenisi Angella Okutoyi, mwanariadha mwenye mbio Zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala, gavana wa Nairobi Jonson Sakaja ni miongoni mwa waliongoza orodha hiyo.

Wengine kutoka Kenya ni Nelly Cheboi aliyepigiwa kura kwenye CNN Heroes, muasisi wa kampuni ya Tech Lit Afrika, mwanaharakati wa mazingira Anita Soina, Elizabeth Wanjiru Wathuti, mwanahabari wa CNN Larry Madowo miongoni mwa wengine.

Je, unahisi ni kwa nini majina makubwa kama Diamond na wenzake wamekosekana kwenye orodha hiyo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved