logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jimal Rohosafi: Mke wangu wa kwanza aliniroga, ndio maana nikawa mjinga

Mfanyibiashara huyo alisema marafiki wa Amira ndio wanamwambia hivyo.

image
na Radio Jambo

Habari16 February 2023 - 04:04

Muhtasari


• Jimal alisisitiza kwamba anajua kile ambacho Amira alikuwa anafuata Tanzania wala si bidhaa za urembo.

• Alisema roho yake sasa imenata kwa Wangari mrembo mpya ambaye amemtambulisha juzi akiwa na ujauzito.

Mfanyibiashara Jimal Rohosafi hatimaye amezungumza maneno ya ukakasi kuhusu mke wake wa kwanza Amira.

Jimal anadai kwamba Amira ni mchawi na mhanga ambaye alimfanyia ulozi na alikuja kuambiwa na rafiki za mke wake huyo.

Uhusiano wa Jimal na mkewe Amira uligonga pabaya miaka mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya kile kilichotajwa kuwa ni kuchepuka na mwanasosholaiti Amber Ray.

Lakini kwa upande wake, Jimal amesema kwamba kutoka kimapenzi na Amber Ray hakukuwa chanzo kikubwa cha kuachana na mke wake wa kwanza bali kulikuwa na suala la ushirikina lililojitokeza.

Jimal alisisitiza kwamba hamsingizii mke wake kwa sababu aliishi naye kwenye ndoa kwa miaka 15 na alikuwa na uhakika wa kile alichokuwa akizungumza.

Alidhibitisha madai yake wiki jana kuwa Amira alienda Tanzania kutafuta zindiko kwa ajili ya kumduwaza Zaidi.

“Kuna nini kingine anafuata Tanzania, mimi siwezi amka asubuhi kama kiongozi nikasema mambo sijui. Amira tumekaa na yeye miaka 15 kwenye ndoa na najua ninachokisema. Ako na marafiki ambao wananipatia tu hadithi zake. Huenda ikawa hata mimi alinipulizia nikawa sijielewi mjinga,” Jimal alisema.

Jimal alisema kwamba wote wale – Amira na Amber Ray wamebaki kama historian a sasa roho yake imenata kwa mrembo Wangari – ambaye alimtambulisha juzi siku ya Valentino akiwa mjamzito.

Alisema kuwa Wangari hivi karibuni atachora tattoo yake ila akadinda kufichua ujauzito wake ni wa miezi mingapi.

“Siwezi waambia uja uzito wake ni wa miezi mingapi, nataka niwape chai pole pole kwa zamu. Mtoto tujajua jinsia yake tayari kila kitu tumemaliza. Roho yangu imependa kwa huyu, ni tattoo bado hajaweka lakini hivi karibuni hilo litafanyika,” Jimal alisema na kudokeza kwamba mengi yatafuata katika siku zijazo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved