logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ramaphosa akataa ombi la mazishi ya kitaifa kwa rapa AKA

Mnamo Alhamisi, Bw Lesufi alisema ombi lake lilikataliwa.

image
na Radio Jambo

Habari17 February 2023 - 07:59

Muhtasari


•Waziri Mkuu wa Gauteng Panyaza Lesufi alikuwa amemwandikia Rais Cyril Ramaphosa akiomba ruhusa ya kumpa AKA mazishi ya kitaifa.

Ombi la utawala wa mkoa kwa ajili ya mazishi ya kiserikali kwa mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini aliyeuawa wiki iliyopita limekataliwa na rais, vinaripoti vyombo vya habari vya ndani .

Waziri Mkuu wa Gauteng Panyaza Lesufi alikuwa amemwandikia Rais Cyril Ramaphosa akiomba ruhusa ya kumpa rapa aliyeuawa Kiernan Forbes, maarufu kama AKA, mazishi ya kitaifa

Mnamo Alhamisi, Bw Lesufi alisema ombi lake lilikataliwa.

Alisema hakuomba fedha za serikali kwa ajili ya mazishi, bali jeneza lifunikwe bendera ya taifa na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya rapa huyo.

"Tulihisi kwamba mtu wa hadhi yake ya kimataifa, mtu wa hadhi ya kitaifa, lazima kuwe na aina fulani ya heshima, na tunataka kufafanua sio mchango wa kifedha," alinukuliwa akisema.

Rapa huyo atazikwa Jumamosi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved