logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tulimzika mtoto wetu Siku ya Wapendanao-Kambua afichua

Kambua alisema mtoto wake alizaliwa Februari 12, 2021.

image
na

Habari01 March 2023 - 11:11

Muhtasari


  • Kambua amemkaribisha bintiye na alimshukuru Mungu kwa baraka zake akisema alikuwa na sababu zote za kumtumikia
Mwinjilisti Kambua

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Kambua amefichua kwamba alimzika mwanawe siku ya wapendanao mwaka wa 2021.

Mama huyo wa watoto watatu alichapisha kwenye Instagram yake alipokuwa akitangaza mradi wake mpya unaoitwa 'Ametenda Mema' ambapo anamshukuru Mungu kwa kuwa mwema katika maisha yake.

Mwimbaji huyo alisema mwezi wa Februari unatakiwa kuwa mwezi wa giza kwake lakini anachagua kusherehekea zaidi yale ambayo Mungu amempa.

Kambua alisema mtoto wake alizaliwa Februari 12, 2021.

"Alifanya mengi zaidi kwa ajili yangu. Mwezi wa Februari ni maalum sana kwangu. Nilikuwa na mvulana wa pekee ambaye Mungu alinipa. Alitua tarehe 12 mwaka 2021 na akaenda kuwa na Bwana na tukamlaza tarehe 14,” alisema.

Kambua amemkaribisha bintiye na alimshukuru Mungu kwa baraka zake akisema alikuwa na sababu zote za kumtumikia.

“Naendelea kuuponya moyo wangu, sasa natazama nyuma naona mwanamke aliyevunjika moyo akibarikiwa kupita kawaida, mwanamke aliyeitwa tasa kwa kuzaa watoto watatu wa ajabu, mmoja yuko mbinguni kwa Bwana na wawili wako pamoja na sisi."

Katika siku za hivi majuzi, Kambua pia alizungumza kuhusu miaka yake ya nyuma wakati madaktari wake walisema hatazaa watoto na upinzani uliokuja nayo.

"Mungu aliketi nami katika giza langu. Na polepole alianza kuniinua. Alinikumbusha pia kwamba miaka iliyopita nilipokea ripoti ya daktari ambayo alisema siwezi kupata watoto.

Alinikumbusha kwamba wakati ulimwengu ukinidhihaki, Alikuwa na shughuli nyingi akifanya kazi kwa ajili ya wema wangu na utukufu Wake.

Hivi sasa mwanamke mahali fulani amejifunza tu kwamba mwili wake hauna "uwezo" wa kutosha kubeba watoto."

Kambua aliwahimiza wale wanaosubiri kubarikiwa na watoto wamngojee Mungu kwani Atawarejesha.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved