logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sokwe wenye njaa wavamia shule Kajiado, wawapiga wasichana na kuiba chakula

Kwa bahati nzuri, mwalimu mkuu alisema, hakukuwa na visa vya majeraha makubwa.

image
na

Habari13 March 2023 - 11:26

Muhtasari


•Sokwe wapatao 200 waliteka' ghala la chakula la Shule ya Sekondari ya Kimana Girls, bustani na jikoni.

•"Wasichana wangu wamepoteza sare na nguo zingine kwa nyani hawa watisha. Ni wanyama wenye vurugu,” alisema mwalimu mkuu.

Kundi la sokwe wapatao 200 waliteka' ghala la chakula la Shule ya Sekondari ya Kimana Girls, bustani na jikoni.

"Waliwapiga wasichana, kwenye mabweni yao walipokuwa wakitafuta chakula. Tumetuma wafanyikazi wetu kupigana nao, lakini wanawazidi idadi,” Catherine Mwaniki, mkuu wa shule hiyo alisema Jumatatu.

Kwa bahati nzuri, mwalimu mkuu alisema, hakukuwa na visa vya majeraha makubwa.

Mwaniki alisema kutokana na ukame uliopo, uhaba wa chakula na gharama ya juu, shule yake inahitaji uingiliaji kati wa Shirika la Huduma za Wanyamapori la Kenya.

Shule hiyo, ambayo iko umbali wa kilomita tatu kutoka ukuta wa mbuga ya wanyama ya Tsavo/Amboseli, pia hutembelewa na ndovu ambao wameharibu takriban asilimia 70 ya uzio wake.

“Nyani ni kero kwa kweli, huwanyang’anya wanafunzi chakula, nguo na pia uharibifu katika shamba la shule. Hatuwezi kufungua mabweni wakati wa mchana kwa sababui ya hewa kuingia, wao huingia ndani na kuacha wameharibu,” Mwaniki alisema.

Alisema nyani hao huenda shuleni kwa sababu wanaweza kupata chakula, mabaki na mazao ya chakula kutoka shambani pia..

"Wasichana wangu wamepoteza sare na nguo zingine kwa nyani hawa watisha. Ni wanyama wenye vurugu,” alisema mkuu wa shule.

Afisa wa KWS wa Loitokitok, Abdi Aden, alisema uzio wa umeme hauwezi kuzuia nyani na tumbili kuingia shuleni kwa sababu wanaruka kutoka kwenye miti hadi kwenye boma la shule.

“Tunafahamu uvamizi huo na ninawasiliana na makao makuu yetu ili kuona namna bora ya kusaidia shule. Chaguo jingine ni kiongozi wao. Kwa tembo, hakika tunahitaji uzio wa umeme,” afisa huyo wa KWS alisema.

Aden alisema anafahamu shule hiyo imepata hasara kubwa kuanzia jikoni, usumbufu darasani, na uharibifu wa shamba.

Mwalimu mkuu alisema ndovu hao wametembelea shule hiyo mara tano tangu Juni mwaka jana, lakini nyani hutembelea taasisi hiyo angalau mara tatu kwa siku.

"Tuna zaidi ya wasichana 600 shuleni wa kulisha, na kwa zaidi ya nyani 200 wanaotembelea mara tatu, ninasikitika kwa sababu gharama zetu za kuwaendeleza wanafunzi shuleni zinapanda," Mwaniki alisema.

Utafsiri: Samuel Maina


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved