logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Mchezaji wa Sunderland ampiga busu yule wa Norwich uwanjani mechi ikiendelea

Baadhi walihisi kitendo hicho kingeangaziwa zaidi ya FA.

image
na Radio Jambo

Habari13 March 2023 - 11:51

Muhtasari


• Shirikisho la soka Uingereza FA halijawahi weka wazi msimamo wake kuhusu LGBTQ.

Tukio lqa ajabu lilishuhudiwa katika ligi ya Champonship nchini Uingereza katika mechi iliyowakutanisha Norwich dhidi ya Sunderland.

Katika mechi hiyo, wachezaji wawili walionekana waking’ang’ania mpira na baada ya wote kuukosa mpira ule, walisukumana hadi nje na kupigana mabusu.

Katika video ambayo imekuwa ikisambazwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii, wachezaji hao wawili walionekana wakisukumana vikali huku kila mmoja akijaribu kudhibiti na kuwahi umiliki wa mpira.

Mechi hiyo ilikuwa inachezewa uwanja wa nyumbani wa Norwich, Carrow Road na kiungo wa timu ya nyumbani Jacob Sorensen alionekana akisukumana vikali na beki wa Sunderland Luke O’Nien.

Wawili hao walisukumana hadi karibu nje ya pembe za chaki ambapo wakati Sorensen anamkaribia O’Nien kwa kichwa, beki huyo alijibu kwa kumnyooshea midomo yake na kumpa busu la haraka kabla ya video hiyo kutamatishwa.

Lakini ilionekana mchezaji yule wa Norwich hakufurahishwa na kitendo kile na kimshikilia kwa nguvu beki O’Nien kwa shingo kama yule anayetaka kumnyonga, ila haijulikana tukio hilo lilikamilika aje kwani video ilitamatishwa.

Mechi hiyo iliyoonekana kuwa na ushindani mkali wa kukata na shoka ilikamilika kwa Sunderland kupata ushindu finyu wa bao moja kapa.

Baadhi walihisi kitendo hicho kingeangaziwa Zaidi na mamlaka zitoe tamko lao, kwani haijawahi zungumziwa hadharani na mamlaka ya soka Uingereza kuhusu msimamo wao katika suala zima linalochemka kote ulimwenguni na LGBTQ.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved