logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa uzuri wako nikiku'cheat nitapata laana ya milele - Maneno ya Billnass kwa Nandy

Mwenyezi Mungu aniongoze ❤️ Nakupenda Mpaka Nakupenda tena ❤️” - Billnass.

image
na Radio Jambo

Habari20 March 2023 - 10:18

Muhtasari


• Nandy na Billnass walioana mwaka jana katika harusi iliyosimamiwa na kanisa na kamati ya Steven Nyerere.

• Mpaka sasa, wapenzi hao wana mtoto mmoja ambaye hawajawahi kumuonesha mitandaoni.

Nandy ashauri wanaume kuwakopa wanawake hela.

Mwanamuziki Billnass amemsifia kwa makopa mke wake Nandy baada ya msanii huyo kupakia picha yake ya kuonesha urembo wake.

Billnass hakuchelewa kufika katika chapisho hilo la mke wake Nandy na kumpa ahadi kwamba kwa uzuri alio nao, ikatokea amemsaliti kimapenzi kwa kuchepuka nje ya ndoa basi itakuwa sawa na kujitafutia laana ya milele.

Billnass alisema kwamba katu hatokuja kumsaliti mpenzi wake hata siku moja na kuliweka ombi hilo mikononi mwa Mungu ili alifanikishe.

Kwa Uzuri Huu Nikikucheat Nitapata Laana ya Milele 🙌🏿 Mwenyezi Mungu aniongoze ️ Nakupenda Mpaka Nakupenda tena ️” aliandika mkali huyo anayezidi kutamba kwa kibao cha Puuh akimshirikisha Jay Melody.

Nandy na Billnass walifunga ndoa mwaka jana huku Nandy akiwa mjamzito na siku chache baadae akajifungua mtoto ambaye hata siku moja hajawahi kumuonesha kwa jamii ya wafuasi wake mitandaoni.

Nandy na Billnass waliapa kutomfungulia mtoto wao akaunti hata moja mitandaoni, katika kile walisema kwamba hawawezi kurubuniwa na usasa wa ‘kumtangaza’ mtoto wao mitandaoni.

Alisema kwamba atasubiri hadi mtoto awe mtu mzima na kufanya uamuzi wa iwapo atajiunga mwenyewe katika mitandao ya kijamii au la.

Hata hivyo, kumekuwa na uvumi kutoka kwa baadhi kwamba huenda hawana huyo mtoto lakini Nandy akapuuzilia mbali dhana hiyo akisema kwamba kila mahali alipo ndipo kuna mtoto wake, ila tu hajawahi muonyesha hadharani mitandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved