logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ripoti ya uchunguzi yabaini uzembe wa marubani katika ajali ya Precision,Tanzania

Ripoti ilisema marubani hawakuwa makini katika kufuata ishara za tahadhari zilizotolewa,

image
na Radio Jambo

Habari23 March 2023 - 05:14

Muhtasari


• Ripoti ya awali ya ilibainisha kuwa kulikuwa na ucheleweshwaji katika uokozi kwa jeshi la Wana maji kufika katika eneo la tukio.

Tanzania imetoa ripoti ya pili ya ajali ya Ndege ya Precision Air iliyotokea tarehe 6 Novemba ,mwaka 2022 katika Ziwa Victoria, Bukoba, Mkoa wa Kagera na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 kuokolewa.

Ndege ya Precision Air iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Bukoba ilikuwa na watu 43 kati yao, 39 abiria, marubani wawili na wahudumu wawili.

Ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air, ilitoka mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022, na ilibainisha kuwa kulikuwa na ucheleweshwaji katika uokozi kwa jeshi la Wana maji kuchelewa kufika katika eneo la tukio.

Vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa ripoti mpya iliyotoka Jumatano imeelezea kuwa marubani wa ndege hawakuwa na tatizo la kiafya, ndege ilikuwa imeandikishwa kihalali, hali ya hewa ya katika uwanja wa Bukoba haikuwa nzuri, hali mbaya ya hewa iliathiri marubani kutekeleza jukumu lao.

Vilevile marubani hawakuwa makini katika kufuata ishara za tahadhari zilizotolewa, ndege iligonga kwanza bawa lake la kushoto wakati ikianguka, pia ilianguka kwa kasi na kugonga sehemu ya mbele kwenye kina cha maji ya ziwa Victoria na vifaa vyote vya kuongozea ndege vilikuwa vinafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya rubani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved