logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maua Sama aomba ushauri sehemu ya mwili atakayochora tattoo, mashabiki wamshauri hivi

Mashabiki wake walimshauri sehemu za ajabu mwilini mwake kuweka tattoo.

image
na Radio Jambo

Habari30 March 2023 - 05:59

Muhtasari


• Hata hivyo, wengine walimshauri kutochora tattoo, wakisema kwamba wanamkubali jinsi alivyo.

Maua Sama aomba ushauri kuchora tatoo.

Moja kati ya wasanii wachache wa kike ambao wanajitahidi sana kujinafasi katika tasnia yenye ushindani mkali ya Bongo Fleva ni mwanadada Maua Sama – mrembo aliyetamba mwaka 2018 na kibao cha ‘iokote’ akimshirikisha Hanstone.

Msanii huyo sasa anataka kuchorwa tattoo mwilini mwake, lakini kabla ya kufanya hivyo, ameamua kuwashirikisha mashabiki wake, ambao muda wote anawaita kama waajiri wake kwenye Sanaa ya muziki.

“Rafiki zangu nichagulie sehemu ya kuweka tattoo,” Sama aliuliza.

Sama kupitia Instastories zake, aliwataka mashabiki wake kumpa ushauri wa sehemu ya mwili amnbayo wangependwa kuona amechorwa tattoo, na majibu ya mashabiki wake ni ya kuchekesha ajabu.

Baadhi walimwambia achore tattoo kwenye panda la uso, wengine wakitaka aichore kwenye mkono, puani, kifuani na sehemu zingine za ajabu.

Hata hivyo, wengine walipinga hatua hiyo, wakimshauri kutokurupuka na kujichora tattoo, kwani jinsi alivyo bila tattoo ako sawa na wanamkubali vivyo hivyo.

“Usiweke, uko vizuri na wa kipekee jinsi ulivyo, msanii wa pekee Tanzania asiye na uchafu mwilini mwake, heshima kubwa sana,” mmoja alimwambia.

Mashabiki wengine walimtaka kutochora tattoo wakidai kuwa wanajifunza kutoka kwake kitu kwani wengi wanamchukulia kama kielelezo cha tabia njema kwenye jamii ambayo wasanii wengi wanatafuta kiki kwa kufanya mambo hata wasiyoyapenda mradi tu kuwafurahisha mashabiki wao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved