logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ MO afunguka kwa nini yeye na mkewe Size 8 hawakuwepo katika harusi ya Akothee

Tulikuwa mbali na tulirudi kwa kuchelewa,” DJ Mo alisema, akidhibitisha kwa kadi.

image
na Radio Jambo

Habari11 April 2023 - 11:33

Muhtasari


•Wasanii wengine pia ambao walialikwa lakini hawakuhudhuria ni Wahu ambaye pia alisema mtoto wake Shiru alikuwa mgonjwa ndio maana hakuhudhuria.

DJ Mo asimulia kwa nini hawakutokea kwa harusi ya Akothee

Mwimbaji Akothee Jumatatu alikuwa na shughuli kubwa ambapo alileta pamoja watu wa tabaka mbalimbali kwenye sherehe ya harusi yake.

Watu mashuhuri wengi wamekuwa wakionyesha picha na video kutoka kwa tukio hilo.

Waliohudhuria harusi hiyo walikuwa wanasiasa wakuu, wafanyabiashara, wanahabari miongoni mwa wengine.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliokosa harusi hiyo ni rafiki wa karibu wa Akothee, The Murayas (DJ Mo na Size 8 Reborn).

Watu wengi wamekuwa wakiibua maswali mengi kuhusu kukosekana kwa wanandoa hao maarufu mitandanoni, huku baadhi wakihisi kwamab huenda kulikuwa na samu mbaya au kutoelewana kwa njia Fulani baina yao na Akothee.

Hata hivyo, DJ Mo kupitia instastory yake, amenyoosha maelezo kuhusu hilo akisema kwamba watu wengi wana maswali yasiyo na maana.

DJ Mo hata hivyo aliweka wazi kwamba Akothee aliwapa mwaliko wa kipekee lakini hawangeweza kuhudhuria, akisema kuwa walikuwa mbali na Nairobi na walifika jijini kwa kuchelewa sana, hivyo hawangeweza kuhudhuria harusi hiyo.

“Watu na maswali tu, ndio tulialikwa lakini hatukuwa karibu. Tulikuwa mbali na tulirudi kwa kuchelewa,” DJ Mo alisema, akidhibitisha kwa kadi hiyo ya mwaliko kwa harusi ya Akothee.

Wahu pia alituma salamu za pongezi kwa wanandoa hao. Alisema hangeweza kuhudhuria harusi hiyo kwa kuwa mtoto wake mdogo alikuwa mgonjwa.

“Rafiki yangu mrembo @akotheekenya na @misteromosh …nyinyi wawili mnastahili furaha yote duniani! Hapa tunawatakia baraka zote za Mungu mnapoanza safari hii nzuri pamoja. Ninajisikia vibaya kwa kutoweza kuhudhuria kwani bosi wangu mdogo Miss Shi hayuko sawa. Pamoja nanyi katika roho, na kukushangilia unapoanza safari yako ya milele pamoja! Hapa ni kwa Mr & Bibi Omosh! 🥂🍾🥂,” Wahu alisema kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii.

Wanamtandao wanaodadisi pia wameona kuwa dadake Akothee Cebbie hakuchapisha chochote kuhusiana na harusi hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved