logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Leroy Sane amuombea msamaha Sadio Mane kwa uongozi wa Bayern, "Msimfukuze tafadhali!"

Mane alisimamishwa kwa muda usiojulikana kwa kumpiga ngumi ya mdomoni Sane.

image
na Radio Jambo

Habari14 April 2023 - 11:32

Muhtasari


• Jarida la BILD liliripoti kwamba Sane na Mane walikuwepo kwenye mkutano uliofanyika kati ya mabosi wa klabu hiyo Alhamisi asubuhi.

• Winga huyo wa zamani wa Liverpool, 31, alisimamishwa na klabu hiyo Alhamisi baada ya yeye na Sane kufanya mkutano na wakuu wa Bayern.

Sadio Mane adaiwa kumpiga ngumi mdomoni Leroy Sane.

Nyota wa Bayern Munich, Leroy Sane ameripotiwa kuwataka wakuu wa klabu kutomfukuza mwenzake Sadio Mane - licha ya kupigwa ngumi na nyota huyo wa Senegal katika mfululizo wa hasira baada ya kushindwa na Manchester City.

Mane alimpiga mwenzake ngumi ya mdomo baada ya kushindwa kwao kwa kishindo na City katika mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Etihad Jumanne.

Winga huyo wa zamani wa Liverpool, 31, alisimamishwa na klabu hiyo Alhamisi baada ya yeye na Sane kufanya mkutano na wakuu wa Bayern.

Kulikuwa na ripoti kwamba Wakuu wa Bayern, Oliver Kahn na Hasan Salihamidžić walikuwa wanafikiria kumfukuza Mane kwa kitendo chake, lakini inaonekana mustakabali wake wa hivi karibuni nchini Ujerumani unaweza kuokolewa na mchezaji mwenza Sane.

Kwa mujibu wa BILD, Sane aliiomba klabu hiyo isisitishe mkataba wa Mane na kuomba winga huyo asipewe 'adhabu kali'.

Pia wanadai kwamba, kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 'mada sasa imefungwa'.

Jarida hilohilo la Ujerumani liliripoti kwamba Sane na Mane walikuwepo kwenye mkutano uliofanyika kati ya mabosi wa klabu hiyo Alhamisi asubuhi.

Muda mfupi baadaye, wachezaji wote wawili walionekana wakishiriki kwenye mazoezi ya timu na walionekana wakikimbia umbali wa mita kutoka kwa kila mmoja.

Saa chache baada ya picha hizo kutokea, klabu hiyo ilitangaza uamuzi wao wa kumsimamisha fowadi huyo. 'Sadio Mané, 31, hatakuwepo kwenye kikosi cha FC Bayern kwa ajili ya mchezo wa nyumbani dhidi ya 1899 Hoffenheim Jumamosi ijayo,' Bayern walisema.

'Sababu ni utovu wa nidhamu wa Mane baada ya mechi ya FC Bayern ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City. Aidha, Mane atapokea faini.'

Mzozo huo uliohusisha nyota hao wawili wa Bayern ulifanyika katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya Bayern kushindwa 3-0 na City.

Sane na Mane walikabiliana walipokuwa wakitoka nje ya uwanja kwenye Uwanja wa Etihad na mzozo ulizidi kuchemka waliposhuka kwenye handaki.

Wakati mzozo ukiendelea hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo, Mane alimpiga ngumi Mjerumani huyo na kumwacha akiwa na mdomo ukiwa na damu, kabla ya wawili hao kuvurugwa kutoka kwa kila mmoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved