logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mahaba bungeni!Mbunge wa Mathira Eric wa Mumbi kumuoa mwakilishi kike wa Murang'a Betty Maina

Siku ya hafla hiyo muhimu kwa wawili hao haijatajwa.

image
na Radio Jambo

Habari18 April 2023 - 13:00

Muhtasari


  • Gachagua ndiye atawaongoza wajumbe wa Mathira katika hafla ya kujadili mahari huku upande wa Maina ukiongozwa na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Mbunge wa Mathira Eric Wa Mumbi na Mwakilishi wa Kike katika kaunti ya Murang'a Betty Maina wanatarajiwa kufanya harusi ya kipekee itakayohudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Gachagua ndiye atawaongoza wajumbe wa Mathira katika hafla ya kujadili mahari huku upande wa Maina ukiongozwa na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Wawili hao kwa sasa wanaishi pamoja, huku wakiadhimisha miaka 2 ya kuwa pamoja.

Siku ya hafla hiyo muhimu kwa wawili hao haijatajwa.

Habari hizi njema zilithibitishwa na Eric Wa Mumbi wakati wa mahojiano na Inooro TV siku ya Jumatatu, Aprili 18. 

"Sasa tumeamua kuishi pamoja kama mume na mke na Bw Gachagua atakuwa kiongozi wa ujumbe wangu wa posa wakati ambapo Mathira itakutana na Murang'a kuchukua binti wao," alithibitisha Mumbi.

Mumbi alifichua kwamba alikutana na Betty mwaka wa 2021, na kugundua kuwa alikuwa kila kitu alichokihitaji katika mke.

Kulingana na mbunge huyo, walianza kuchumbiana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2022, na walikubaliana kuanza kuishi pamoja.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved