logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baadhi ya Waislamu walaani taarifa kuhusu Eid kutoka kwa serikali ya Kenya

Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameishutumu serikali ya Kenya kwa kuwapotosha watu

image
na Radio Jambo

Habari21 April 2023 - 13:58

Muhtasari


•Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Kithure Kindiki alitangaza Jumatano kwamba Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid.

•Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameandika kwenye mitandao ya kijamii kulaani hatua ya serikali.

Wasomi wa Kiislamu wamesema kuwa mwisho wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan unapaswa kutangazwa na KadhiImage

Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameishutumu serikali ya Kenya kwa kuwapotosha watu baada ya kutangaza kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid al-Fitr.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Kithure Kindiki alitangaza Jumatano kwamba Ijumaa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya Eid.

Mwenyekiti wa Baraza kuu la Waislamu nchini Kenya (Supkem) Hassan Ole Naado, ambaye alizungumza na gazeti la Nation, alisema kuwa tangazo la serikali linawakanganya Waislamu nchini humo, kwani uamuzi wa siku ya Eid hutegemea muonekano wa mwezi.

Bw. Naado alisema kuwa: "Serikali inafaa kuomba ushauri Waislamu kabla ya kufanya uamuzi. Hili ni kosa kubwa na upotoshaji,” alisema.

Baadhi ya Waislamu nchini Kenya wameandika kwenye mitandao ya kijamii kulaani hatua ya serikali.

Eid al-Fitr ni sikukuu muhimu kwa Waislamu, ya kuadhimisha mwisho wa mwezi wa Ramadhani, ukiwa ni mwezi wa tisa katika historia ya Kiislamu.

Mara kwa mara Waislamu wamekuwa wakitofautiana kuhusu siku ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani, baadhi wakiuona mwezi kabla ya wengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved