logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Naweza kukata simu?" Mwanadada mkali amuuliza Gidi baada ya kumkana mumewe

"Nilishaachana na mambo yake. Hata simjui. Nimesema simjui," Irene alisema.

image
na Radio Jambo

Habari25 April 2023 - 05:30

Muhtasari


•Collins alisema mke wake alimwambia watengane baada ya kuenda nyumbani kwao takriban mwezi mmoja uliopita.

•Irene aliweka wazi kwamba hataki uhusiano na Collins na kumuomba aache kumfuatilia kwa mahusiano.

Gidi na Ghost

Collins ,30, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Irene ,23, ambaye alimtema ghafla bila kutoa sababu yoyote.

Collins alisema mke wake alimwambia watengane baada ya kuenda nyumbani kwao takriban mwezi mmoja uliopita.

"Mke wangu ni mchezaji mpira. Kuna siku ameenda Nakuru. Yeye huwa na ugonjwa wa asthma. Baada ya kutoka Nakuru alikuja akiwa mgonjwa sana. Niliongea na yeye akasema ameenda nyumbani kwa sababu baba yake ni daktari," Collins alisimulia.

Aliongeza, "Baada ya wiki moja nilimpigia simu akaniambia niachane na yeye. Baadaye aliniweka blacklist. Rafiki yake alimwambia nilikuwa namtafuta akanitoa blacklist. Baada ya kunitoa blacklist tulizungumza."

Collins alieleza kuwa huenda kuna jamaa anamtongoza mkewe kwani alipigiwa simu akasikia sauti ya mwanaume.

"Jana kuna mwanaume alinipigia simu na simu ya mke wangu, aliaanza kunitusi akisema mimi ni mjinga.. Nilijaribu kuzungumza na yeye, tukabishana hatukuelewana," alisema.

Collins alikana kuwahi kumkosea mpenzi huyo wake wa mwaka mmoja wala kumpiga.

Irene alipopigiwa simu alikana kabisa kumfahamu Collins.

"Nilishaachana na mambo yake. Hata simjui. Nimesema simjui," alisema.

Collins hata hivyo alibainisha kwamba wanajuana na hata walikuwa wamezungumza kwa simu asubuhi.

Irene aliweka wazi kwamba hataki uhusiano na Collins na kumuomba aache kumfuatilia kwa mahusiano.

"Simjui na sitaki mambo yake. Mwambie sitaki mambo yake. Nishamwambia. Mbona awapigie simu na nimemwambia simtaki," alisema.

Gidi alijaribu kumuomba aeleze sababu ya kuchukua msimamo huo mkali lakini akaomba kukata simu.

"Naweza kata hii simu," Irene aliuliza kabla ya kutoweka kwenye laini.

Simu ya Collins pia ilikatika na hivyo wawili hao hawakuweza kupatana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved