logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Mzungu hawezi kukutosheleza', Andrew Kibe amwambia Akothee

Akothee alimsuta Kibe kwa kukosa heshima kwa wanawake akidai hana uwezo kimapenzi.

image
na

Habari27 April 2023 - 05:30

Muhtasari


 

•Kibe aliongezea kuwa mwanaume mzungu hana uwezo wa kutosheleza mwanamke wa kiafrika na kuwa mwanaume mwafrika ndiye ana uwezo huo.

 

Akothee na Andrew Kibe wakabana koo.

Mwanavlogu Andrew Kibe, anayeishi Marekani  amemrushia vijembe Akothee akisema kuwa mahusiano yake si ya kweli.

Katika vlogu yake kwenye Facebook, Kibe ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwakashifu mastaa wa Kenya alisema kuwa iwapo Akothee angetaka kutoshelezwa kimapenzi basi atafute Mwafrika na si mzungu.

"Ukitaka mwafrika sema kwa sababu mzungu hawezi kukutosheleza,ukiona hauko sawa nikonyezee jicho,nitajipanga," alisema Kibe

Kibe aliongezea kuwa mwanamume mzungu hana uwezo wa kutosheleza mwanamke wa kiafrika na kuwa mwanaume mwafrika ndiye ana uwezo huo.

Hivi majuzi Akothee na Andrew Kibe wamekuwa katika mzozo mtandaoni tangu Akothee alipofunga ndoa. Akothee kwa hamaki alimsuta Andrew Kibe kwa kile alichodai ni kukosa heshima kwa wanawake.

Akothee alisema kuwa Kibe hana hata uwezo wa kumtongoza kwa sababu ana upungufu wa shughuli za unyumba kwa sababu ya kubugia pombe. Alisema anatia sumu kizazi hiki na mawaidha yake potovu.

Akothee na mume wake kutoka Uswizi ,Dennis Schweizer, walifanya harusi ya kifahari katika hoteli ya Windsor jijini Nairobi iliyohudhuriwa na mastaa na wanasiasa akiwemo Mama Ida Odinga. Mama huyo wa watoto watano alisema kuwa atafanya harusi ya pili nchini Switzerland na ataenda pamoja na wasimamizi wake wote.

Andrew Kibe amejipata katika ugomvi na maceleb wengi nchini Kenya, anajulikana kwa kuwasuta kila mara. Baadhi yao ni kama vile Diana B na Bahati,Terence Creative, Willy Paul na wengineo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved