logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mke wa Samidoh, Edday Nderitu apakia picha akiwa na ujauzito, watu wacharuka

Baada ya kupakia, aliwaacha watu wakibishana kuhusu picha hiyo.

image
na Radio Jambo

Habari28 April 2023 - 08:16

Muhtasari


• Baadhi walisema ni picha ya mimba ya zamani huku wengine wakiendelea mbele na kumhongera kwa mimba ya mtoto wa nne.

Edday Nderitu atokea na muonekano mpya akiwa na mimba.

Edday Nderitu, mke wa kwanza wa Samidoh amewaacha wanamitandao vinywa wazi baada ya kupakia picha akiwa na ujauzito na kusema kuwa hakuna hisia nzuri kama zile za kujua unabeba kiumbe mwilini mwako.

Katika picha hiyo ambayo haijulikani kama alikuwa anarejelea uzito wa zamani ama wa sasa hivi, Nderitu alionekana ameshikilia tumbo lake kwa upendo na kusema kwamba hakuna zawadi kubwa kuliko ya mama kugundua kuwa ana mimba.

“Ni kiumbe chenye nguvu zaidi kuwa na maisha yanayokua ndani yako. Hakuna zawadi kubwa Zaidi kuliko mimba,” Nderitu aliandika.

Baadhi ya mashabiki kwenye sehemu ya maoni walidai picha hiyo ilipigwa kitambo Edday akiwa na ujauzito wa bintiye wa mwaka mmoja huku wengine wakiendelea kumpongeza mama huyo wa watoto watatu kwa kupata mimba ya mtoto wa nne.

“Eeeh bana...Samidoh anafaa kutuonesha njia zake...sisi hatuna nguvu 😂😂 ni kama nyota ya wanaume ilipewa samidoh..hata hivyo sisi Tunangoja mimba yetu na Karen nyamu..team karenzo..Eddy anakaa kimaguta,” mmoja kwa jina Tonnie Henrys alisema.

“Hongera Edday...wewe ongeza watoto bora mtu wa mkono wa kupea samidoh connection senator Karen Nyamu, Youth President ako... zaaa mama hizo pesa za senate lea nazo watoto,” mwingine alimpa ushauri tata.

“Kabisa, asante Mungu kwa akina mama wote kwa kubeba uhai matumboni mwao. Ninaonekana mwenzetu mpendwa 🐐 Mke na Mwenyekiti wetu wa Global wa 🐐 Wake. Bwana akulinde kwa ajili ya kizazi hiki kwa jina la Yesu. Makamu Mwenyekiti wako aliyeteuliwa anafurahi unapokuwa,” Wairimu Kimani alisema.

Hata hivyo, haijulikani ukweli wa picha hiyo na Nderitu mwenyewe hajatoa maelezo Zaidi kama kweli ni mimba ya mtoto wan ne au ni kumbukumbu ya mimba ya tatu.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved