logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arteta awaomba mashabiki wa Arsenal kumheshimu straika wa Chelsea, Aubameyang

"Alikuwa mchezaji wa ajabu kwetu, alifunga mabao mengi, alikuwa nahodha wetu, na anastahili hilo.”

image
na Radio Jambo

Habari02 May 2023 - 08:40

Muhtasari


• Licha ya tofauti zao, Arteta amesisitiza kwamba ipo haja kwa Aubameyang kuoneshwa heshima anaporejea Emirates usiku wa leo.

Mikel Arteta wa Arsenal

Jumanne usiku kutakuwa na mechi kubwa ya debi baina ya mahasimu wawili kutoka jiji la London, Arsenal wakimenyana na Chelsea katika uga wa Emirates.

Huku pande hizo zikiwa na historia ndefu ya kubadilishana wachezaji, kocha wa Arsenal Mikel Arteta amewaomba mashabiki wake kumpa heshimu za juu mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang amabye alikuwa mchezaji wao kabla ya kuondoka kwenda Barcelona na kisha kurejea ligi ya premia safari hii akiitumikia Chelsea.

Aubameyang ambaye alikuwa nahodha wa Arsenal aliondoka Emirate kishari baada ya kutofautiana na kocha Arteta na safari hii kwa mara ya kwanza atarejea huko kama mchezaji wa timu pinzani.

Mshambulizi huyo wa zamani wa The Gunners anaonekana kwa mara ya kwanza Emirates tangu Arteta aandae ripoti ya makosa yake ya utunzaji wa wakati, akamvua kitambaa hicho na akakatisha mkataba wake na malipo ya pauni milioni 7 miezi 16 iliyopita.

Licha ya tofauti zao, Arteta amesisitiza kwamba ipo haja kwa Aubameyang kuoneshwa heshima anaporejea Emirates usiku wa leo.

Arteta alisema: “Wacha tuseme asante, tupe heshima na shukrani kwa kile alivyokuwa. Alikuwa mchezaji wa ajabu kwetu, alifunga mabao mengi, alikuwa nahodha wetu, na anastahili hilo.”

The Gunners watarejea kileleni mwa Ligi ya Premia ikiwa wataendeleza mbio za kutoshinda kwa The Blues hadi mechi tisa. Na Arteta anadai kuwa mbio za ubingwa hazijaisha, akiwaonya viongozi Manchester City.

“Nikiangalia hili halijaisha, bado tunaweza kufikia Ligi Kuu kwa sababu kuna mechi tano zimebaki na mambo mengi yatafanyika, ningelipa pesa nyingi msimu ujao ili niwepo katika nafasi hii tuliyo sasa, niamini.”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved