logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwigizaji katika shoo ya “Njoro wa Uba” na mchekeshaji Ochonjo aaga

Tasnia ya ucheshi nchini Kenya ina huzuni mkubwa kufuatia kifo cha ghafla cha Ochonjo Dunco.

image
na

Habari11 May 2023 - 09:04

Muhtasari


• Habari hizo za kusikitisha zilitangazwa na mwigizaji Sandra Dacha.

• “PUMZIKA KWA AMANI rafiki na mwenzangu @ochonjodunco 🙏🏿,” Sandra alisema.

Mcheshi Mike Wako na rafiki yake Ochonjo

Mcheshi na muigizaji maarufu Tony Ochonjo Dunco ameaga dunia. “Njoro wa Uba” Mwigizaji na mchekeshaji Ochonjo aaga

Ochonjo ambaye alikuwa muigizaji katika kipindi cha 'Njoro wa Uba'  alikuwa pia maarufu kwenye TikTok kwa video zakeakiwa na wacheshi wenza Osongo na Mike Kwako.

Wadau katika taaluma ya uchekeshaji nchini Kenya wanaomboleza kifo cha ghafla cha mcheshi na mwigizaji Ochonjo Dunco.

Habari hizo za kusikitisha zilitangazwa na mwigizaji Sandra Dacha. Dacha aliyehuzunika alisimulia jinsi ilivyo vigumu kukubaliana na kifo cha ghafla cha Ochonjo.

"Maisha ni ya kupendeza. KIFO ni amani. Ni mpito huo ambao unasumbua.” Dacha aliandika katika akaunti yake ya Instagram.

“PUMZIKA KWA AMANI rafiki na mwenzangu @ochonjodunco 🙏🏿,” Sandra alisema.

Dacha alifichua kuwa Ochonjo alilazwa hospitalini Alhamisi wiki jana. Na aliaga leo saa 2 asubuhi.

“Siku kama hii wiki iliyopita ndipo tulipokupeleka hospitali… Mwenzangu @ochonjodunco alivuta pumzi yake ya mwisho saa 2 asubuhi leo😭”

 

“10/5/2023. Unakumbatia kifo kwa sababu maisha hayapo bila wewe. Umeacha kumbukumbu nzuri ambazo hazitafifia mioyoni mwetu. Hadi tutakapokutana tena pumzika kwa amani Ochos🕊️🕊️🕊️🕊️🕊️🕊️🕊️,” ilisoma sehemu ya chapisho y Sandra Dacha.

 

Wakenya kutoka matabaka mbalimbali walijiunga na mazungumzo hayo wakionyesha mshtuko kwa kifo hicho cha ghafla huku wakimuomboleza mchekeshaji huyo.

Ochonjo pia alikua maarufu katika mtandaowa  TikTok kwa video yake na wacheshi wachanga Osongo na Mike Wako.

Click here to edit this text.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved