logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ramsdale aongeza mkataba wa kudumu katika Arsenal

Ramsdale mwenye 25, amefungwa mabao 40 katika mechi 36, akiwa Arsenal kwenye ligi.

image
na

Habari19 May 2023 - 07:29

Muhtasari


•Kipa wa Arsenal Aaron Christopher Ramsdale ametia sahihi ya  mkataba wa kudumu kuendelea kuitumikia timu hiyo.

•Ramsdale alijiunga na Arsenal mwaka wa 2021 kutoka Shiffield United kwa kim cha pauni milioni ishirini na nne  ndipo kufanikisha na kuwakilisha majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na Bernd Leno aliyeondoka zake Fulham kusaka zaidi muda wa kucheza.

Kipa wa Arsenal Aaron Christopher Ramsdale ametia sahihi ya  mkataba wa kudumu kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Ramsdale alijiunga na Arsenal mwaka wa 2021 kutoka Shiffield United kwa kima cha pauni milioni ishirini kuchukuwa majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na Bernd Leno aliyeondoka zake Fulham kusaka zaidi muda wa kucheza.

Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 25, tangu ajiunge na vigogo hao wa soka amefungwa mabao arubaini katika mechi thelathini na sita kwenye ligi kuu nchini Uingereza msimu huu wa 2022/2023 na kutofungwa mara kumi na tatu kila anapoonekana kwenye lango.

Mlinda lango huyo amekuwa nguzo muhimu katika ufanisi wa Arsenal msimu huu chini ya ukufunzi wa Mikel Arteta.

Arsenal katika mtandao wao wa kijamii walisema;

″Tuna furaha kwa kuwa Aaron ameongeza mkataba mpya.Jinsi Aaron amekuwa akinawiri kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita  ni wa kipekee, utendakazi wake na namna alivyokabiliana na mashambulizi  pia.″

Meneja wa timu Mikel Arteta alieleza;

″Ni vyema pia kuwa, tunaendelea kunawirisha timu yetu kwa kutumia talanta murua kutoka kwa kikundi chetu,tunatazamia kumwona Aaron akitumikia klabu hii katika miaka mingi ijayo.″ Aliendelea. 

Ramsdale aliongeza kuwa, muda wa miaka miwili kwake pia imekuwa ya kufana zaidi, na cha msingi ni kutulia na kuacha kiburi akitumai kuwa miaka mingine michache ijayo ataweza kufanikisha azma ya Arsenal. 

Arsenal, ambao wapo katika nambari ya pili kwenye ligi kuu uingereza,nyuma ya bingwa mtetezi Man City, watakuwa na kibarua wikendi hii dhidi ya Nottingham Forest katika mechi itakayobaini bingwa wa ligi msimu huu. Iwapo watashinda,na Man City kupoteza mikononi mwa Chelsea basi ligi itachukua mkondo mwingine.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved