logo

NOW ON AIR

Listen in Live

China yakanusha kuwa ilidukua mashirika ya serikali ya Kenya

siku ya Jumatano, ubalozi wa China ulisema ripoti hiyo "ni potofu na upuuzi mtupu".

image
na Radio Jambo

Habari25 May 2023 - 08:42

Muhtasari


• Shirika la habari la Reuters lilikuwa limeripoti kuwa mashambulizi ya mtandaoni ya miaka mingi yalianza mwaka wa 2019.

Shirika la habari la Reuters lilikuwa limeripoti kuwa mashambulizi ya mtandaoni ya miaka mingi yalianza mwaka wa 2019 wakati Wachina walipoanza kufungia Kenya mikopo.

Ubalozi wa China nchini Kenya umekanusha ripoti ya shirika la habari la Reuters kwamba wadukuzi kutoka taifa hilo la Asia walishambulia mashirika muhimu ya serikali jijini Nairobi, ikiwa ni pamoja na ofisi ya rais, ili kutathmini iwapo nchi hiyo italipa mabilioni ya dola inayodaiwa na Beijing.

Shirika la habari la Reuters lilikuwa limeripoti kuwa mashambulizi ya mtandaoni ya miaka mingi yalianza mwaka wa 2019 wakati Wachina walipoanza kufunga njia za mkopo kwa Kenya huku matatizo ya deni yakianza kuonekana.

Lakini katika taarifa siku ya Jumatano, ubalozi wa China ulisema ripoti hiyo "ni potofu na upuuzi mtupu".

"Udukuzi ni tishio la kawaida kwa nchi zote na China pia ni mwathirika wa mashambulizi ya mtandao," iliongeza.

Ubalozi unasema ni suala nyeti sana la kisiasa kulaumu serikali fulani kwa shambulio la mtandao bila ushahidi thabiti.

Inasema uhusiano kati ya Kenya na China unatokana na kuheshimiana.

Kenya imeripotiwa kupunguza kukopa kutoka China na kufikia Machi ilidaiwa na nchi hiyo ya kusini-mashariki mwa Asia $6.31bn (£5.8bn).


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved