logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mulamwah na mpenziwe watimba TTNT 4 kibabe, wapewa ulinzi mkali na mabouncer

Njugush na Wakavinya walikuwa wanazindua msimu wa nne wa simulizi ya maisha yao, TTNT.

image
na Radio Jambo

Habari28 May 2023 - 07:15

Muhtasari


• Mabouncer hao ambao kwa muonekano wao wamenyanyua vyuma vya kutosha, misuli imesitunya na kusinyaa huku wakiwa vifua wazi.

Jinsi Mulamwah na mpenzi wake Ruth K walitimba kwenye TTNT msimu wa 4 ya Njugush na mkewe Wakavinya.

Usiku wa Jumamosi mchekeshaji Njugush na mpenzi wake wa muda mrefu Wakavinya walikuwa wanazindua mwendelezo wa filamu ya maisha yao, msimu wa nne maarufu Through Thick & Thin, TTNT katika ukumbi wa KICC.

Katika hafla hiyo kubwa ambayo ilifanikishwa na jinsi sehemu ya kwanza hadi tatu zilivyopata mapokezi ya kibabe na mashabiki wao, Njugush aliwaalika watu maarufu kadhaa wa humu nchini na wengi wao walijitokeza kwa mitindo ya aina yake kusimama na mwenzao kwenye Sanaa ya burudani.

Licha ya maceleb wengi kujitokeza kwa mionekano ya kupapasa hali ya hewa, Mulamwah na mpenzi wake Ruth K walismamisha jiji, huku kila mmoja akiwazungumzia jinsi walivyotimba kwenye hafla hiyo kwa njia ya kibabe mno.

Wakiwa wamevalia Nadhifu, Mulamwah walitembea kwa mwendo wa madaha, huku mikono imegandiana kwa mapenzi na nyuma yao wanapewa ulinzi mzito na mabouncer wawili kila upande.

Mabouncer hao ambao kwa muonekano wao wamenyanyua vyuma vya kutosha, misuli imesitunya na kusinyaa huku wakiwa vifua wazi, walitoa ulinzi wa VIP kwa wapenzi hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilificha penzi lao kwa kujitania kuwa ni marafiki tu – bestee bestee.

Mulamwah ambaye Jumapili amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiadhimisha miaka 30 tangu kutua duniani alitania kuwa walivalia suti wakati hafla yenyewe ilikuwa imewataka kuvalia mavazi ya kimjini mjini.

“Kijana wa birthday ndio kuingia KICC TTNT4 na bestee Ruth K, nasikia mavazi huku ni ya kimjini na mimi nilikuwa nimevalia suti ya siku ya kuzaliwa,” Mulamwah alitania.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved