logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rick Ross afurahishwa na urembo wa Ayra Star

Rick Ross alimsifia Ayra Star kaika video akisema ni mrembo na mwenye kipaji.

image
na

Habari02 June 2023 - 07:31

Muhtasari


• Rick Ross pia aliongeza kuwa atakapotembelea nchi hiyo ya Nigeria angependa kumwona Ayra na kufanya sherehe naye.

• Video hiyo imeibua gumzo mitandaoni huku wafuasi wa wasanii hao wakihisi ni kama Rick Ross alitaka kuwa na mahusiano na mwanamziki huyo tajika.

Rick Ross na Ayra Starr.

Staa wa ngoma za Rap kutoka Marekani, William Leonard Roberts II, maarufu kwa jina la Rick Ross amevutiwa na urembo wa mwanamziki wa Nigeria Ayra Starr.

Katika video aliyochapisha kwenye akaunti yake ya Insagram Rick Ross alimsifia Ayra akisema kwamba alikuwa mrembo na mwenye kipaji.

“Ni mimi hapa Rick Ross, nataka kumtambua msanii Ayra Starr, wewe ni mrembo na wewe ni msanii mkubwa na bosi kama mimi.”alisema Rick Ross.

Rick Ross pia aliongeza kuwa atakapotembelea nchi hiyo ya Nigeria angependa kumwona Ayra na kufanya sherehe naye.

“Nikija Nigeria tutasherehekea kama mabosi, shikilia papo hapo na endelea kupiga kazi safi,”

Video hiyo imeibua gumzo mitandaoni huku wafuasi wa wasanii hao wakihisi ni kama Rick Ross alitaka kuwa na mahusiano na mwanamziki huyo tajika.

Mwaka wa 2022 Rapa huyo mwenye umri wa miaka 46 alithibitisha uhusiano wake na mpenzi wa zamani wa msanii wa Diamond Platinumz,Hamisa Mobetto.

Wawili hao walionekana katika video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii wakiwa Dubai, Hamisa alipokuwa mapumzikoni baada ya kuwa marafiki kwa muda mrefu.

Huko Dubai, Rick Ross alishindwa kujizuia kumwonyesha mama huyo wa watoto 2 kwa sababu ya urembo wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved