logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sam Allardyce aondoka Leeds baada ya kushindwa kuisaidia kusalia katika EPL

Leeds ilitangaza kwamba tangazo la kocha mpya litatolewa katika wiki zijazo.

image
na Radio Jambo

Habari02 June 2023 - 09:19

Muhtasari


•Allardyce alitoa shukran kwa klabu hiyo kwa kumpa nafasi ya kutoa huduma ya ukufunzi katika hatua ya mwisho mwisho ya msimu.

•Allardyce alijiunga na Leeds mwanzoni mwa mwezi Mei baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Javi Garcia.

ameondoka Leeds baada ya mwezi mmoja.

Leeds United imethibitisha kwamba kocha wake Sam Allardyce ataondoka katika klabu hiyo kufuatia mwisho wa msimu wa 2022/23.

Katika taarifa yake ya siku ya Ijumaa, klabu hiyo ambayo ilishushwa daraja kutoka EPL baada ya kumaliza msimu katika nafasi ya 19 kwa pointi 31 ilibainisha kuwa Allardyce anaondoka kufuatia makubaliano ya pande zote.

"Leeds United na Sam Allardyce wanaweza kuthibitisha kuwa pande zote mbili zimekubaliana kwa pamoja kwamba muda wa Sam katika klabu kumalizika baada ya kukamilika kwa msimu wa 2022/23," taarifa ya klabu hiyo ilisema.

Allardyce alitoa shukran kwa klabu hiyo kwa kumpa nafasi ya kutoa huduma ya ukufunzi katika hatua ya mwisho mwisho ya msimu.

Ingawa hakufanikiwa kusaidia Leeds kutoshushwa daraja, kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 alisema alifurahia kushirikiana na wafanyikazi na wachezaji katika kipindi chake cha mwezi mmoja alichokuwa katika klabu hiyo.

"Katika hatua hii ya maisha yangu, sina uhakika kuchukua changamoto hii, ambayo inaweza kuwa mradi wa muda mrefu, ni kitu ambacho naweza kujitolea, lakini naitakia kilabu mafanikio kwa siku zijazo na ninatumai klabu itarejea katika Ligi Kuu, mahali ambapo wanastahili," Sam Allardyce alisema.

Leeds ilitangaza kwamba tangazo la kocha mpya litatolewa katika wiki zijazo.

Allardyce alijiunga na Leeds mwanzoni mwa mwezi Mei baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Javi Garcia.

Allardyce alikuwa kocha wa tatu kusimamia Leeds United katika msimu wa 2022/23. Makocha wawili wa hapo awali, Garcia na Marsch walitimuliwa kufuatia msururu wa matokeop hafifu katika mechi za Ligi Kuu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved