logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mpenziwe Wema Sepetu afunguka kuhusu hofu yake kubwa iliyomfanya kuwa mwaminifu kwake

Whozu alisema mojawapo ya hofu zake kubwa ni kumkosea mpenziwe na hivyo hawezi kupata ujasiri wa kumsaliti kimapenzi.

image
na Radio Jambo

Habari03 June 2023 - 12:46

Muhtasari


•Whozu alisema mojawapo ya hofu zake kubwa ni kumkosea mpenziwe na hivyo hawezi kupata ujasiri wa kumsaliti kimapenzi.

•Whozu alibainisha kwamba mahusiano yake wa sasa yameundwa na mapenzi  mazito ya pande zote mbili.

Mwanamuziki wa Bongo Oscar John Lelo almaarufu Whozu amekiri kwamba amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na muigizaji Wema Sepetu.

Akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alibainisha kwamba mahusiano yake wa sasa yameundwa na mapenzi  mazito ya pande zote mbili.

"Sasa hivi niko kwenye mapenzi mazito sana. Mwanamke niliye naye, Wema Sepetu ananipenda sana, na mimi ninampenda sana. Napendwa," Whozu alijigamba.

Aliongeza, "Nikifa leo, katika wasifu ambao mtasoma, msisahau kusema eti nilipenda sana." 

Whozu aliweka wazi kwamba hajawahi kumsaliti Wema kimapenzi tangu walipojitosa katika mahusiano zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Alieleza kwamba mojawapo ya hofu zake kubwa maishani ni kumkosea muigizaji huyo na hivyo hawezi kupata ujasiri wa kumsaliti kimapenzi.

"Mwanamkewangu ni wa kwanza ninayeogopa kumkosea kwa chochote kile, ata kumhusu kwa kitu kidogo ninaogopa, sembuse kumcheat? siwezi!  Nina mwaka sijacheat. Mimi sijui kucheat. Kucheat ya nini," Whozu alisema.

Wema na Whozu walijitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka uliopita baada ya kuwa marafiki kwa muda mrefu.

Mapema mwaka huu, muigizaji huyo alifunguka jinsi alivyokutana na Whozu na hatimaye kuanza kuchumbiana mwaka jana.

"Tulikuwa Dodoma, nilikuwa nimeenda kwa ajili ya kazi. Yeye alikuwa amefika kwa ajili ya masuala yake mwenyewe," Wema Sepetu alisema wakati wa kikao cha Iftar nyumbani kwake mnamo mwezi Aprili mwaka huu.

Alisema baada ya kukutana mwaka wa 2019 walishiriki uhusiano wa kirafiki kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mwaka jana.

"Tumekuwa marafiki. Wakati mwingine nilikuwa namshauri kwenye mambo yake ya mapenzi. Tulianza kuchumbiana mwezi wa nne mwaka jana," alisema

Mwimbaji Whozu alikuwa kwenye mahusiano mengine wakati alipokutana na muigizaji huyo na kuanza urafiki.

Sepetu hata hivyo ameeleza kuwa mahusiano ya awali ya mchumba huyo wake tayari yalikuwa yamefika kikomo walipoanza uchumba.

"Alikuwa na shida zake yeye na mtu wake. Mimi sikutaka kuingilia. Nilikuwa wa msaada kwa namna moja ama nyingine pale ambapo alihitaji sapoti. Tulikuwa naye kama rafiki kwa miaka miwili. Niseme nini, jambo moja lilipelekea jingine.. sijawahi kuvuruga mahusiano ya watu. Tukianza mahusiano alikuwa single sana. Alikuwa bila mchumba kwa takriban miezi mitano," alisema muigizaji huyo.

Wawili hao waliweka mahusiano yao wazi mwaka jana wakati mpenzi huyo wa zamani wa Diamond akiadhimisha siku ya kuzaliwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved