logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mke wangu alimkodishia mume wake wa pili nyumba karibu na kwangu-Mwanamume asimulia machungu yake

Wakati wao walipa ndoa heshima zake, na kila mmoja kujua majukumu yake katika familia.

image
na Radio Jambo

Habari09 June 2023 - 13:41

Muhtasari


  • Wengi wanaanza ndoa kwa sababu amemuona mwenzake amefunga pingu a maisha bila kujua na kufahamu ndoa ni mkataba wa milele.
Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.

Kwa kweli akina babu zetu wakieza amka na kutazama dunia na karne hii jinsi ilivyo hawawezi tamani kuishi au kuitwa akina babu zetu.

Wakati wao walipa ndoa heshima zake, na kila mmoja kujua majukumu yake katika familia.

Ndio wengi wamesema kwamba kizazi hiki kimeoza, na kwamba hakina heshima na hata hakiheshimu tamaduni.

Wengi wanaanza ndoa kwa sababu amemuona mwenzake amefunga pingu a maisha bila kujua na kufahamu ndoa ni mkataba wa milele.

Haya yanashuhudiwa na jinsi wanandoa wengi wanapeana talaka hata kabla ya kuishi miaka mingi.

Mwanamume mmoja aliwaacha wanamitandao midomo wazi baada ya kufichua kwa uchungu kile mke wake amekuwa akifanya, na kusingizia anaenda kanisani.

Huu hapa usimulizi wake;

"Mara ya kwanza nilimpata mke wangu akiwa na mwanamume mwingine kitandani, alienda kisha nikamsamehe,baada ya kurudi aliniahidi kwamba amebadilika 

kila siku alikuwa anaenda kanisani katika ibada za jioni,hii aliniambia ilikuwa ishara ya kuwa amebadilika na kwamba anataka kuwa karibu na Mungu ili ndoa yetu iweze kuimarika."

Baada ya muda bwana huyo aligundua kipi ?, aliendela;

"Baada ya muda niligundua kwamba mke wangu alikuwa amemkodishia mume wake wa pili nyumba karibu na tulipokuwa tunaishi,kmbe ibada ya kanisa ambapo alikuwa anaenda alikuwa anaenda kukutana na mwanamume huyo."

Je nni kinapaswa kufanywa ili karne na kizazi hiki cha sasa kiweze kuheshimu tamaduni na ndoa.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved