logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwalimu Rachael ajutia kuwa meneja wa kundi la Sailors

Mwalimu Rachael alishutumiwa na wafuasi wa kundi hilo kwa kunyakuwa akaunti ya YouTube ya Sailor.

image
na

Habari09 June 2023 - 06:55

Muhtasari


• Mwalimu Rachel alisema kusimamia Sailors ni majuto yake makubwa maishani hadi sasa.

• Mwalimu Racheal alikemewa kwa madai ya kuwa kizuizi kwa taaluma ya vijana hao, tuhuma ambazo alikanusha. 

Kundi la Sailors na meneja wao wa zamani, Mwalimu Rachael.

Mcheshi Mwalimu Rachel ameelezea kujutia kusimamia kundi maarufu la muziki wa Gengetone, Sailors.

Katika video aliyopakia kwenye akaunti yake ya Instagram Mwalimu Rachel alisema kusimamia Sailors ulikuwa uamuzi  wa kujutia maishani hadi sasa.

Katika mahojiano hayo Mwalimu Rachel alifichua sababu ya kutengana na kundi hilo ilikuwa kwa ya kutoelewana na wanachama.

Mwalimu Rachael alishutumiwa na wafuasi wa kundi hilo kwa kunyakuwa akaunti ya YouTube ya Sailor.

Kutokana na dhana ya wafuasi wa Sailors, mtangazaji huyo alikiri kuwa  yeye na mwanawe walipokea vitisho vya kuuawa mtandaoni.

“Vitisho ambavyo nimekumbana navyo mtandaoni imenitikisa sana. Mimi na mwanangu tumepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa mashabiki kwa sababu ya chaneli hiyo ya YouTube,” alisema Mwalimu Rachael.

Mwalimu Racheal alikemewa kwa madai ya kuwa kizuizi kwa taaluma ya wanamziki hao, tuhuma ambazo alipinga vikali.

"Sikuua taaluma yao. Huenda watu wanafikiria nilifanya hivyo, na wamefikia hatua ya kuwataka mabosi  wangu wanifukuze kazi, licha ya kutojua lolote kuhusu kisa cha kweli.”

Kikundi hicho cha muziki kilijumuisha Peter Miracle Baby, Shalkido, Cocos Juma, Masilver na Lexxy Yung.

Kundi hilo lilipata umaarufu na wimbo wao Wamblambez mwaka wa 2018 wakati mtindo wa  Gengetone ulivuma kote nchini ya Afrika Mashariki. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved