logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Utacheka alichoambiwa Harmonize na Rotimi kuhusu Vanessa Mdee, Jux asahaulika!

“Warembo wengi sana hapa kaka ila dada yenu ni rafiki wangu mkubwa,” Harmonize aliandika

image
na Radio Jambo

Habari30 June 2023 - 04:39

Muhtasari


• Wawili hao walifurahia kukutana kama watu ambao wamejuana kwa muda mrefu huku Harmonize akionekana kupigana vibega na msanii Rotimi.

Harmonize akiwa na Rotimi Marekani.

Katika misele ya ziara yake ya muziki nchini Marekani, msanii kutoka Konde Gang, Harmonize amekutaka kwa ghafla na msanii Rotimi, ambaye ni shemeji wa ukanda wa Afrika Mashariki.

Harmonize alipakia video hiyo wakiwa wanasalimiana kwa kukumbatiana na mume huyo wa msanii Vanessa Mdee ambaye ni mpenzi wa zamani wa Juma Jux, msanii na mjasiriamali wa chapa ya African Boy.

Kwenye Video hiyo, Harmonize aliweka wazi kwamba alikuwa katika jimbo la Los Angels ambalo linatajwa kuwa kitovu cha Sanaa kutoka filamu hadi muziki na wote ni kama walikuwa wageni kwenye hafla moja – kumbuka Rotimi ni mkaaji wa jimbo la Atlanta.

Wawili hao walifurahia kukutana kama watu ambao wamejuana kwa muda mrefu huku Harmonize akionekana kupigana vibega na msanii Rotimi na kuandika maneno ya kumtania.

“Warembo wengi sana hapa kaka ila dada yenu ni rafiki wangu mkubwa,” Harmonize aliandika, akionekana kunukuu maneno aliyoambiwa na Rotimi wakati wa gumzo lao fupi.

Katika ziara yake Marekani, Harmonize amesifiwa pakubwa kwa kuendelea kutengeneza urafiki na connections na mibabe wa Sanaa ambao wanatajwa kuwa ndio kusema katika sekta mbalimbali za burudani nchini Marekani.

Tangu Rotimi na Vanessa Mdee waoane miaka michache iliyopita na kubarikiwa na watoto wawili kwa haraka, msanii huyo hajawahi onekana akiwa na msanii yeyote kutoka Tanzania, ambao kiuhalisia ni kama taifa la mashemeji zake.

Harmonize ndiye alikuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kuonekana na Rotimi tangu kumchukua Vanessa kutoka kwenye mikono na Jux.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved