logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gavana Anyang' Nyong'o ajawa bashasha kwa kukutana na binti yake Lupita Nyong'o Ufaransa

Nyong'o alibainisha kuwa kushiriki muda na familia yake kila mara humpa furaha tele ndani ya moyo.

image
na Radio Jambo

Habari06 July 2023 - 07:15

Muhtasari


•Nyong'o alionyesha picha yake na muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 wakiwa wametulia katika eneo zuri katika jiji hilo zuri barani Ulaya.

•Muigizaji huyo maarufu wa Kenya na Canada ni mmoja wa watoto wa gavana Anyan’g Nyong'o na mke wake Dorcas Nyong'o. 

nchini Ufaransa siku ya Jumatano.

Gavana wa Kisumu Peter Anyang' Nyong'o mnamo Jumatano alikutana na binti yake mrembo Lupita Nyong'o jijini Paris, Ufaransa.

Nyong'o alifichua maelezo ya mkutano huo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo alionyesha picha yake na muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 wakiwa wametulia katika eneo zuri katika jiji hilo zuri barani Ulaya.

Gavana huyo wa chama cha ODM alibainisha kuwa kushiriki muda na familia yake kila mara humpa furaha tele ndani ya moyo.

"Katika mkutano na binti yangu @Lupita_Nyongo jijini Paris. Ni vyema kila wakati kuwa na wakati na familia yangu," Gavana Nyong'o alisema siku ya Jumatano.

Lupita Nyong’o hata hivyo hakushiriki maelezo yoyote ya mkutano wake na babake kwenye kurasa zake za mitandao mbalimbali ya kijamii.

Muigizaji huyo maarufu wa Kenya na Canada ni mmoja wa watoto wa gavana Anyan’g Nyong'o na mke wake Dorcas Nyong'o. Wengine ni pamoja na Peter Nyong'o Junior na Zawadi Nyong'o. Lupita anajulikana sana kwa kushiriki katika filamu za kimataifa kama vile Black Panther, 12 years a Slave, Star Wars, The 355 miongoni mwa zingine.

Muigizaji huyo Hollywood alimtambulisha mpenzi wake hadharani kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana.

Lupita alimtambulisha mtangazaji wa televisheni Selema Masekela kama mpenzi wake  kupitia video nzuri ambayo alipakia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. 

Katika video hiyo, wapenzi hao walionekana wakiwa wamevalia mavazi tofauti yanayofanana huku wakicheza kwa vidole vyao.

"Tunaingiana tu 💖 @selema #thisismylove  #nuffsaid, (Huyu ni mpenzi wangu, yamesemwa ya kutosha," Lupita aliandika chini ya video hiyo fupi ambayo alichapisha kwenye  Instagram siku ya Ijumaa.

Selema ambaye ni mtangazaji na mwimbaji wa Marekani alithibitisha kuwa Lupita Nyong'o ni mpenzi wake wa kweli.

"Mioyo imeshikamana. Mpenzi wangu kamili na halisi @lupitanyongo❤❤❤," aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Selema Masekela , 51, ni mwandishi wa habari za michezo na pia ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya mavazi  ya Mami Wata.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved