logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wapenzi wanaswa wakila uroda kwenye madhebahu Uganda, Waumini wadinda kuingia kanisani hadi litakaswe

Wakaazi wadinda kutosali katika Kanisa moja baada ya wapenzi kunaswa ndani wakila uroda.

image
na

Habari07 July 2023 - 08:47

Muhtasari


• Viongozi wa kanisa hilo katika Kata Ndogo ya Kayonza Wilaya ya Kayonza sasa wanasema wameingia katika idadi isiyojulikana ya siku za kufunga na sala.

• Kwa mujibu wa kiongozi huyo wapenzi hao waliweza kuingia katika kanisa hilo kupitia madirisha kwa sababu milango ilikuwa imefungwa.

Kanisa

Wakaazi wa wilaya ya Bugonya nchini Uganda wameapa kutosali katika Kanisa moja katika eneo hilo baada ya wanandoa kupatikina wakishiriki tendo la ndoa kwenye madhabahu ya kanisa hilo.

Viongozi wa kanisa hilo katika Kata Ndogo ya Kayonza Wilaya ya Kayonza sasa wanasema wameingia katika idadi isiyojulikana ya siku za kufunga na sala kufuatia kile walichokielezea kuwa ni kitendo cha kushtua.

Siku ya Jumatano, wenyeji waliiambia tovuti ya Monitor kwamba wataepuka kanisa hilo hadi viongozi wake waandae misa maalum ya kusafisha "kitendo cha kishetani kilichotokea nyumbani kwa Mungu Jumanne mwendo wa saa 8 jioni."

Mwenyekiti wa Bugonya IC1 George William Kanda alieleza kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kijiji chake aliingia kanisani na mwanamke Muislamu kupitia dirisha.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wapenzi hao waliweza kuingia katika kanisa hilo kupitia madirisha kwa sababu milango ilikuwa imefungwa.

"Walifika kanisani kupitia madirisha sababu milango wa kanisa ilikuwa imefungwa," Kanda alisema.

Cha kushangaza Zaidi ni kuwaWawili hawa hawakuwa washirika wa kanisa hilo bali wanakijiji katika eneo hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved