logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu ombaomba tajiri zaidi duniani mwenye thamani ya shilingi milioni 141

Bharat Jain ambaye kazi yake kuu ni kuomba omba ametajwa kuwa ‘mwombaji tajiri zaidi duniani’ .

image
na

Habari14 July 2023 - 04:38

Muhtasari


• Kulingana na gazeti la Economic Times, Bharat Jain hakumudu kupata elimu yoyote na akaamua kuomba-omba ili kupata riziki.

• Watoto wake, kwa upande mwingine, hawatafuata nyayo zake. Tayari wamemaliza elimu yao na ata kupata ajira nchini humo.

Omba Omba tajiri

Mwanaume mmoja wa India ambaye kazi yake kuu ni kuwaomba watu pesa kwenye mitaa ya Mumbai ametajwa kuwa ‘mwombaji tajiri zaidi duniani’ na vyombo vya habari vya India vinavyodai kuwa ana thamani ya zaidi ya dola milioni moja.

Wakati watu wengi nchini India wanataabika kwa saa nyingi kila siku kwa ajili ya rupia mia chache, Bharat Jain, anayeitwa ‘mwombaji tajiri zaidi duniani’, anaripotiwa kutengeneza kati ya rupia 2,000 na 2,500 kila siku kwa kuwaomba pesa watu wakarimu.

Jain amekuwa akiomba katika maeneo yenye shughuli nyingi Mumbai kama vile kituo cha reli cha Chatrapati Shivaji Maharaj Terminus (CSMT) au Azad Maidan kwa miaka mingi sasa na amejikusanyia pesa nyingi.

Thamani yake ya jumla inatarajiwa kuwa karibu 7.5 crore (milioni Sh 141.4), na inajumuisha gorofa ya vyumba 2 huko Mumbai yenye thamani ya crore 1.2, na maduka mawili huko Thane ambayo yanakodisha rupia 30,000 kwa mwezi.

Mapato yake ya kila mwezi yanakadiriwa kutofautiana kati ya rupia 60,000 (Sh 102,846.92) na rupia 75,000 (Sh 119,643.55 ), ambayo inaonekana ni zaidi ya Wahindi wengi walioajiriwa hupata.

Kulingana na gazeti la Economic Times, Bharat Jain hakumudu kupata elimu yoyote na akaamua kuomba-omba ili kupata riziki.

Watoto wake, kwa upande mwingine, hawatafuata nyayo zake. Tayari wamemaliza elimu yao na ata kupata ajira nchini humo.

Familia ya Jain inamshauri kila mara kuacha kuombaomba kwani wanaweza kumudu kuishi bila kulazimika kuomba mitaani, lakini hilo halitakuwa kizuizi kwa kazi yake anayoienzi.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved