logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kama dem wako alikuwa kwenye tafrija ya usiku ya Diamond, kaka hauna dem" - Nay

Nay aliwataja warembo hao kuwa mangandu wa mjini tu ambao hawafai kuolewa.

image
na Radio Jambo

Habari17 July 2023 - 07:02

Muhtasari


• Kwa maneno haya, Nay alimaanisha kwamba vipusa waliojitokeza kwenye tafrija hiyo walionesha tabia Fulani ya kukera.

Diamond na Jux wapondwa kwa kuandaa tafrija usiku na warembo nusu uchi

Usiku wa kuamkia Jumapili msanii Diamond Platnumz na mwenzake Juma Jux waliandaa kile kiliitwa ‘House Party’ wakiwaalika watu mbali mbali kufurahia wimbo wao mpya wa ‘Enjoy’.

Wawili hao walionekana usiku wakiwa ndani ya gari la Diamond wakiingia kweney sehemu ya ukumbi wa sherehe hiyo ambayo ilikuwa na watu wengi walioalikwa kwa nyama choma, kujivinjari kwa kupiga mbizi, kucheza muziki miongoni mwa matukio mengine mengi yaliyopamba tafrija hiyo.

Mashabiki wengi walioonekana katika video zinazosambazwa mitandaoni ni pamoja na wasichana vipusa ambao walikuwa wamevalia katika mitindo ya tafrija za mijini zinazofanyika kwenye kumbi za tafrija gizani.

Kwa jinsi warembo hao walikuwa wanajiachilia, baadhi ya watu mitandaoni wameiponda tafrija hiyo na kusema kwamba ilikuwa ni njia moja ya kugubika anasa kwa jina la ‘House Party’.

Nay wa Mitego, msanii wa kurap kupitia Instagram yake alichokoza akisema kwamba kama wewe ni mwanamume na unajua kwamba mrembo wako alihudhuria kwenye tafrija hiyo basi jua fika kwamba huna mpenzi pale – ni kutupa tu.

“Kama dem wako alikuwa kwenye House Party jana, bro hauna dem hapo. Hilo ni ngandu kama mangandu mengine yua mjini,” Nay alisema.

Kwa maneno haya, Nay alimaanisha kwamba vipusa waliojitokeza kwenye tafrija hiyo walionesha tabia Fulani ya kukera ambayo haiwezi hata kidogo kuwapa nafasi ya kutambulishwa kwenye boma kama watu wa kufunga ndoa naye.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved