logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanawe Martha Karua ajiunga na TV47 baada ya kuondoka KTN News

Mtangazaji huyo wa habari ni mpwa wa Martha Karua lakini mwanasiasa katika siku za nyuma alimtaja kama mwanawe.

image
na Radio Jambo

Habari20 July 2023 - 08:03

Muhtasari


•Maringa  alitangaza kujiunga kwake na TV47 siku ya Jumanne kupitia akaunti zake rasmi za mitandao ya kijamii.

•Mtangazaji huyo wa habari ni mpwa wa Martha Karua lakini mwanasiasa katika siku za nyuma alimtaja kama mwanawe.

Mpwa wa aliyekuwa mgombea mwenza wa Azimio la Umoja-One Kenya Martha Karua, George Maringa amejiunga na kituo cha utangazaji cha TV47, siku chache tu baada ya kuondoka Standard Group.

Maringa ambaye alifanya kazi katika KTN News kwa zaidi ya nusu muongo alitangaza kujiunga kwake na TV47 siku ya Jumanne kupitia akaunti zake rasmi za mitandao ya kijamii.

“Leo usiku, safari mpya inaanza.. Jiunge nami kwenye habari za TV47. The Home of Untold stories,” Maringa alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Aliisindikiza taarifa hiyo na picha zake akiwa kwenye chumba cha habari cha maskani yake mapya.

Baada ya tangazo hilo, msomaji huyo wa habari alijitosa kazini mara moja na kuendelea kuwasilisha habari siku ya Jumanne na Jumatano jioni.

Maringa alitangaza kuondoka Standard Media Group baada ya takriban miaka sita siku ya Jumatatu kupitia kurasa zake rasmi.

Katika tangazo lake, alidokeza kwamba angehamia kazi nyingine.

“Miaka 5, miezi 11.. Asante kwa kutembea nami katika safari. Hadi kazi inayofuata,” Maringa aliandika kwenye mtandao wa Facebook.

Alisindikiza taarifa hiyo na picha yake akiwa nje ya ofisi za Standard Group kando ya barabara ya Mombasa.

Mapema, Julai 2 alifichua kwamba alikuwa ameacha kazi yake katika KTN News Kenya.

Mtangazaji huyo wa habari ni mpwa wa Martha Karua lakini mwanasiasa katika siku za nyuma alimtaja kama mwanawe.

Mwezi Desemba 2021, mgombea mwenza huyo wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana alishiriki picha yake, Maringa na mama yake Lucy Maringa ambaye pia ni dada yake.

"Nikiwa na dada yangu Lucy Maringa na mwanawe George Maringa ambaye ninajivunia kuwaita mwana," Karua aliandika.

Martha Karua ana watoto wawili wakubwa ambao wanapendelea kuweka maisha yao ya faragha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved