logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Niliumia sana-Uhuru asema baada ya polisi kuvamia nyumba ya mwanawe

Kiongozi huyo wa zamani wa nchi alikanusha madai kuwa alikuwa amelewa alipotembelea nyumbani kwa mtoto huyo.

image
na Radio Jambo

Habari24 July 2023 - 13:50

Muhtasari


  • Rais wa nne alisisitiza kwamba wanawe walikuwa na leseni ya wamiliki wa bunduki ambayo ilikusudiwa kuwalinda wao na familia zao.

Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta mnamo Jumatatu, Julai 24, alilalamika kwamba serikali ilijaribu kuwawekea wanawe wawili wa kiume, Jomo Kenyatta, na Muhoho Kenyatta dawa za kulevya na bunduki.

Katika mkutano na wahariri wa habari, Uhuru alifichua kuwa kisa hicho cha Ijumaa usiku kiliumiza hasa baada ya kupokea simu ya huzuni kutoka kwa mwanawe Jomo Kenyatta.

Kiongozi huyo wa zamani wa nchi alikanusha madai kuwa alikuwa amelewa alipotembelea nyumbani kwa mtoto huyo.

Nilikwenda (nyumbani kwa mwanangu) kwa sababu ya simu ya dhiki kutoka kwa mwanangu. Niliumia sana,” Uhuru aliwaambia wahariri.

Mbunge huyo wa zamani wa Gatundu Kusini alilalamika kwamba serikali ilikuwa na lengo la kumpata yeye na familia yake kiasi cha kuondoa usalama wa mamake, Mama Ngina.

Aliongeza kuwa hakuna hata mmoja wao aliyepokea amri yoyote ya kusalimisha bunduki zao kama ilivyodaiwa na serikali na vyombo vya habari.

Katika mahojiano hayo yenye hisia kali, Uhuru alifichua kuwa wanawe wawili, Jomo na Muhoho, walikuwa na bunduki sita pekee na kwamba bintiye Ngina hakuwa na silaha yoyote.

Rais wa nne alisisitiza kwamba wanawe walikuwa na leseni ya wamiliki wa bunduki ambayo ilikusudiwa kuwalinda wao na familia zao.

Kulingana na Uhuru, Jomo alipata leseni baada ya usalama kuondolewa. Kwa upande mwingine, Muhoho alisemekana kupendezwa na bunduki kutokana na shughuli yake ya kurusha ndege katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mwea.

"Ninajua hakuna kifungu cha sheria cha kupanua usalama wa watoto wangu licha ya ombi langu. Kwa hivyo, niliwahimiza kutuma maombi na walifuata taratibu," Uhuru aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved