logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu safari ya mapenzi ya muigizaji Jackie Matubia na Blessing Lung'aho

Jackie na Blessing Lung'aho wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuanzia mwaka wa 2021.

image
na

Habari27 July 2023 - 12:35

Muhtasari


• Wawili hao walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuanzia mwaka wa 2021 baada ya kupatana wakati wa majaribia ya kuigiza katika kipindi cha Zora.

• Jackie ana watoto wawili mmoja wao akiwa wa muigizaji mwenza Blessing.

Jumanne, Jackie Matubia alithibitisha mahusiano yake na muigizaji mwenza Blessing Lung’aho yametamatika baada ya muda wa zaidi ya miezi miwili ya kudokeza kuwa mambo huenda yakawa mabaya katika mahusiano yao.

Muigizaji huyo wa zamani wa kipindi cha Zora akiwaarifu wafuasi wake katika akuanti yake ya Instagram , alisema sasa anajivunia kuwa singo matha.

"Proud single mother of two," Jackie aliandika kwenye instastory yake.

Wawili hawa wamekuwa wakitoa vidokezo vya kila aina kwamba huenda mapenzi yao na baba wa mtoto wake wa pili, Blessing Lung’aho yalivunjika.

Mnamo alhamisi, Jackie alidai kuwa wanaume walimjazia maombi ya kutaka kuwa kwenye mahusano naye baad ya kutangaza kuwa singo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved