logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa Kilifi kuzuiliwa siku 14

Kesi hiyo itatajwa Agosti 17, 2023.

image
na Radio Jambo

Habari27 July 2023 - 12:46

Muhtasari


  • Naliaka, ambaye alifanya kazi kama msaidizi wa nyumba katika nyumba ya marehemu Karisa anasemekana kumdunga kisu bosi wake mnamo Julai 20.

Diana Naliaka, mshukiwa mkuu wa mauaji ya Rahab Karisa, Afisa Mkuu wa Uvuvi na Uchumi wa Bluu katika Kaunti ya Kilifi alifikishwa Alhamisi katika mahakama ya Kilifi.

Hakimu Justus Kituku aliupa upande wa mashtaka siku 14 kumzuilia mshukiwa, ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi wa kisa hicho.

“Nimesikiliza ombi la kiongozi wa mashtaka kuomba muda zaidi kumzuilia mshukiwa ili kukamilisha uchunguzi wao. Sina pingamizi kwa hilo nikizingatia uzito wa kesi hiyo,” akasema hakimu Kituku.

Naliaka, ambaye alifanya kazi kama msaidizi wa nyumba katika nyumba ya marehemu Karisa anasemekana kumdunga kisu bosi wake mnamo Julai 20.

Kisha akakimbilia eneo lisilojulikana.

Mnamo Julai 25, Naliaka alikamatwa Busia na inaaminika alikuwa akikimbilia Uganda.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 17, 2023.

Inadaiwa mtafaruku ulitokea baada ya yeye kurejea nchini kutoka Italia alikohudhuria mkutano muhimu wa kimataifa na akapata pesa zake kiasi fulani zilikuwa zimepotea nyumbani.

Mwanamke huyo anatoka Bungoma na alikuwa amewaambia baadhi ya marafiki zake kwamba alikusudia kuondoka kwenda Uganda kwa muda.

Wachunguzi walisema kuwa Rahab alipata Sh32,000 zikiwa hazipo kati ya Sh100,000 alizokuwa akihifadhi nyumbani kwake.

"Alitafuta majibu kutoka kwa mjakazi pamoja na shangazi yake kuhusu mahali zilipo pesa na kutishia kuwaripoti kwa polisi asubuhi," mpelelezi alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved