logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baadhi ya huduma zilizoathiriwa na jaribio la udukuzi siku ya Alhamisi

Alhamisi, huduma muhimu zinazotolewa na mashirika ya serikali yaliathirika na jaribio la udukuzi.

image
na

Habari28 July 2023 - 10:16

Muhtasari


• Waziri  Eliud Owalo alithibitisha shambulio katika huduma za e-Citizen lakini akasema hakuna data iliyoathiriwa.

Siku ya Alhamisi, huduma muhimu zinazotolewa na mashirika ya serikali ikiwa ni pamoja na tuvuti ya e-Citizen, Huduma za ununuzi wa token za KPLC, shirika la reli nchini, NTSA, Mpesa, Benki ya Standard Chartered na benki ya ABSA yaliathirika na jaribio la udukuzi.

Waziri  Eliud Owalo alithibitisha shambulio katika huduma za e-Citizen lakini akasema hakuna data iliyoathiriwa.

Huduma katika tuvuti hiyo hata hivyo ziliweza kurejeshwa baada ya wataalam akatika wazara ya ICT kuingililia kati.

Alhamisi jioni, Kampuni ya Kenya Power and Lighting ilisema mfumo wake ulikumbwa na hitilafu ya mtandao na kusababisha kutopatikana kwa baadhi ya huduma ikiwa ni pamoja na ununuzi wa token kutumia USSD na Mpesa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved